VAN PERSIE AREJESHWA HARAKA ENGLAND, WENGER ASEMA MSIMAMO ULE ULE HATA NYOTA WOTE WAONDOKE
CHELSEA YAMRUDIA MODRIC
KLABU ya Chelsea imerejea kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo
wa kimataifa wa Croatia, Luka Modric, na Mwenyekiti wa Spurs, Daniel
Levy kwa sasa anashilia funguo za kabati kibao za fedha nyingi kwa ajili
ya mauzo ya mchezaji huyo.
KIUNGO wa Chelsea, Frank Lampard, mwenye umri wa miaka 34, ameonyesha
nia ya kubaki Stamford Bridge licha ya kutakiwa kwa dau nono na LA
Galaxy na klabu nyingine China.
BEKI wa kimataifa wa Hispania, anayechezea Marseille ya Ufaransa, Cesar Azpilicueta, mwenye umri wa miaka 22,
amerejea kwenye mipango ya uhamisho wa Chelsea, kutokana na harakati za
Kocha Roberto Di Matteo kuendelea kusaka beki mpya wa pembeni.
NAHODHA wa Arsenal, Robin van Persie, mwenye umri wa miaka 29, amerejea
England kufanya mazungumzo na kocha wake, Arsene Wenger baada ya kuibuka
hofu kwamba anafanya mpango wa kujiunga na Real Madrid.
KOCHA mpya wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers hana mpango wa kumuuza kiungo wa kimataifa wa Wales, Craig Bellamy.
KLABU ya Stoke City ipo karibu kumsajili beki wa Houston Dynamo, Geoff Cameron, mwenye umri wa miaka 26, ambaye tayari ameichezea mechi tano Marekani.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Denmark, anayechezea wa AAB, mwenye umri wa miaka 21, Nicklas Helenius, ambaye anawaniwa na Norwich, West Brom na Fulham, anaweza kupenda kuhamia Uholanzi au Ujerumani.
MANCINI ATAKIWA URUSI
KOCHA Roberto Mancini amepewa ofa ya pauni Milioni 35 kuikochi
Urusi, wakati mazungumzo yake ya mkataba mpya na klabu yake, Manchester
City yakiendelea.
KOCHA Arsene Wenger amesema atabadilisha mfumo wake wa uendeshaji Arsenal - hata kama wachezaji wake nyota wataendelea kuondoka.
KOCHA Vicente Del Bosque amemkaribisha kocha wa Liverpool,
Brendan Rodgers katika kambi ya Hispania kubadilishana mawazo, kujadili
mipango na falsafa.
KIUNGO Joe Cole ametupilia mbali mpango wa kurejea katika klabu yake ya Liverpool na kuendelea kwenye klabu anayochezea sasa.
BEKI wa Manchester City, Pablo Zabaleta amesema kwamba mchezaji
mwenzake mtata, Mario Balotelli anaweza kuwa mmoja wa wachezaji bora
duniani kama ataanza kutumia akili yake zaidi.
No comments:
Post a Comment