Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, July 3, 2012

UCHAGUZI YANGA KUFANYIKA DIAMOND JUBILEE, WAGOMBEA VYETI UTATA WASHITUKIWA




WAKATI Uchaguzi Mkuu wa Yanga utafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga mjini Dar es Salaam Julai 15, mwaka huu wagombea saba wako hatarini kuenguliwa.
Hao ni Mgombea Uenyekiti, Sara Ramadham na Ujumbe Ramadhan Mzimba ‘Kampira’, Edgar Fongo, Abdallah Mbaraka, Mohamed Mbaraka, Ahmad Waziri Gao na Shaaban Katwila.
Kwa nini? Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu amesema kwamba, Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeagiza wagombea hao wawasilishe vyeti vyao halisi mbele ya Kamati ya Uchaguzi ya Yanga.
“Wanatakiwa hadi Julai 4 wawasilishe vyeti halisi saa 10:00 jioni, na ili kuwapa nafasi hawa kuwasilisha vyeti vyao, muda wa kuanza kampeni sasa umesogezwa mbele hadi Julai 6,”alisema Sendeu, ambaye amedokeza pia kocha mpya wa klabu hiyo, Mbelgiji Thom Saintfiet atawasili kesho.source bin

No comments:

Post a Comment