Askofu
mpya kabisa kutawazwa imearifiwa kuwa anashikiliwa na mamlaka ya Uchina
baada ya kutangaza kuwa anajiuzulu kutoka Kanisa Katoliki
linalokubalika na Mamlaka ya Uchina.
Thaddeus Ma Daqin, Askofu wa
Shanghai, alitangaza hatua yake ya kujiuzulu kutoka Chama kijulikanacho
kama China Patriotic Association (CPA) siku ile ambapo alitawazwa wiki
iliyopita.
Duru za Kanisa Katolika na vyanzo
vingine vya kidini vimesema kuwa kiongozi huyo wa dini anashikiliwa
ndani ya Seminariyo moja karibu na Shanghai.
Kwa mda mrefu kumekuwepo hali ya kutofahamiana baina ya Uchina na Vatican.
Vatican, iliyomteuwa Askofu Ma,
haitambui chama cha CPA kinachokinzana na Kanisa Katoliki na Kanisa
Katoliki nchini Uchina halitambui Mamlaka ya Papa.
Waumini wanaokadiriwa kutimu milioni
10 wa huko Uchina wamegawika kati ya wafuasi wa Papa na upande wa pili
ukikubaliana na kundi la Chinese Patriotic Catholic Association (CPA).
Taarifa zinasema kuwa Askofu Ma
aliuambia ummati wa watu 1,000 kuwa ameamua kujiuzulu ili awezew
kushughulikia majukumu yake mapya. Tangazo lake hilo lilifuatiwa na
makofi ya waumini , kwa mujibu wa habari za gazeti linalochapishwa huko
HongKong la South China Morning Post.
Lakini wadadisi wanasema kuwa hatua
hio ilionekana na wakuu wa Uchina kama kejeli na kudharau udhibiti wa
Dola la Uchina juu ya viongozi wa Kanisa Katoliki na wengine
No comments:
Post a Comment