Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, July 7, 2012

WANYARWANDA WAJA NA MPYA SABASABA



Dr. Emmanueli Sina kutoka Rwanda akiwaonyesha wananchi walipotembelea banda la Wanyarwanda katika maonyesho ya sabasaba namna mashine inayotoa sumu mwilini jinsi invyofanya kazi kwa kutumia mkanda kwa kujifunga tumboni ambao unaunganishwa na mashine kisha mtu kutumbukiza miguu ndani ya beseni na sumu yote kutoka ndani ya mwili kama inavyoonekana katikaka picha.

 

PICHA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE
MTAMBO maalum wa kuondoa sumu mwilini mwa binadamu wagundulika na wananchi wameaswa kuangalia afya zao mara kwa mara kutokana na kula vyakula vyenye kemikali ambazo hutengeneza sumu ndani ya miili yao.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Dk Emmanuel Shoo katika banda la Wanyarwanda kwenye maonesho ya 36 ya biashara ya kimataifa sabasaba katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyrere na kusema kwmba mwili wa binadamu unachukua sumu nyingi kutokana na vyakula vya kisasa.

Alisema kwa watu wanaotumia sigara, pombe na anapovuta moshi wa magari hiyo yote ni hatarikwa afya zao ndio maana wamekuja kuonesha wananchi wa Tanzania mtambo huo ambao huondoa sumu yote mwilini mara  tu mtu anapovalishwa mkanda na kuanza kukamua sumu.

Dk Shoo alisema mashine inapowashwa mtu huvalishwa mkanda tumboni na kasha anaingiza miguu katika beseni lenye maji na kuna kifaa maalum kinaingizwa katika beseni hilo kisha mtambo unaanza kazi yake ya kuondoa sumu yote mwilini na inabakia katika lile beseni.

Aliendelea kwa kusema kwamba ndani ya tumbo ini na figo zote zinasafisha uchafu na mwili wa binadamu unabaki kuwa na hali yake ya kawaida na afya njema.
Alisema kwmba mara baada ya mtu huyo kusafishwa anapewa dawa maalum ya asili ya Kinyarwanda ambayo anakunywa na kisha kutoa uchafu mwingi tumboni na kujisikia vizuri na pia mtu anashauriwa kufanya hivyo mara nne kwa mwaka ili afya yake iimarike zaidi kutokana na vyakula vya kemikali anavyovitumia kila siku.

Dk Shoo alisema kwamba bei ya kusafishwa na mtambo huo kuwa kwa mtu mmoja ni sh 20,000 na wao wapo katika banda la Wanyarwanda kwenye maonesho hayo hivyo amewaasa watanzania kutembelea mahali hapo kuja kujionea namna mtambo huo unavyofanya kazi na wala hauna madhara kwa binadamu.

Akitoa shuhuda jinsi mtambo huo unavyofanya kazi mmoja wa wananchi ambaye alitembelea na kupata huduma katika banda hilo Kabengwi Ndebile Kabwengwen alisema hakika mtambo huo ni mzuri na wanyarwanda wanastahili pongezi na kuiasa serikali kununua vifaa vyake ili kuvisambaza vijijini kuwaokoa wazee waliopatwa na matatizo ya mgongo na magoti.

No comments:

Post a Comment