Pages

Friday, July 6, 2012

WATANZANIA, HII NDIO TAARIFA MPYA KUHUSU MTANZANIA HASHEEM THABEET.



Nataka utambue kwamba Timu maarufu iliyofika mpaka kwenye fainali ya ligi ya NBA nchini Marekani na kutolewa na Miami Heat hivi karibuni Oklahoma City Thunder imekubali kusaini mkataba wa miaka miwili na mchezaji wa mpira wa kikapu Mtanzania Hasheem Thabeet.
Sababu tatu za Oklahoma kumchukua Hasheem… kwanza ni sababu za kifedha, yani Hasheem ni mchezaji mkubwa ambae ameshamaliza mkataba wake na timu aliyokua anaichezea, na Oklahoma wameweza kumpata kwa bei wanayoweza kuilipa ndio maana.

Kama hufahamu ni kwamba tangu Hasheem alipotoka collage kuingia NBA, Oklahoma ndio ilikua timu ya kwanza kumtaka ila Memphis ambao walikua na nafasi ya kuchagua wachezaji wapya kabla ya Oklahoma wakamchukua kwa hofu kwamba kama wangemuacha angechukuliwa na Oklahoma.
Kingine ambacho inawezekana haukifaham ni kwamba Oklahoma inawachezaji watatu sasa hivi ambao Heiden, Igbuka na Perkins ambao msimu uliopita walikua tegemezi kubwa sana kwenye hii timu na kwa vyovyote vile watadai pesa ndefu kwenye mikataba yao mipya mwaka huu.

No comments:

Post a Comment