WEMA
Isaac Sepetu amelidokeza gazeti alipendalo la Ijumaa Wikienda kuwa
ameitwa ikulu ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza kwa mwaliko maalum. Wema
alisema mwaliko huo aliupata mara tu baada ya kuzindua ile filamu yake
ya Super Star wiki mbili zilizopita ambapo katika mwaliko huo wa ujumbe
kutoka ikulu hiyo ulimuomba kutoisambaza kwanza kabla ya kwenda
kuizindua nchini humo. “Waliniambia
juu ya mimi kuomba uraia wa nchi hiyo ili kukuza filamu zao. Kusema
kweli nilikuwa nina ratiba ya kwenda kuizindua filamu yangu Rwanda,
Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Yaani sijui hata walijuaje.
Sijui ni nini kimetokea, nina wasiwasi. Hata sijui nitaongea nini na
Rais wa Burundi,” alisema Wema na kuongeza kuwa maandalizi yakikamilika
atatii wito huo muda wowote HABARI NI KWA NIABA YA AMANI MASUE |
No comments:
Post a Comment