Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, July 10, 2012

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAJIPANGA KUTOKA HUDUMA ZA UZAZI BURE


NA KHADIJA KHAMIS –IDARA YA HABARI MAELEZO
Wizara ya Afya Zanzibar imejipanga kutoa huduma zote za uzazi bure kwa wananchi zikiwemo zile za upasuaji zitafanyika bila ya malipo kuanzia mwaka wa fedha 2012 na  kuendalea.

Hayo yameelezwa leo huko katika ukumbi wa baraza la wawakilishi nje kidogo na mji wa Zanzibar ,wakati akiwasilisha hotuba ya waziri wa afya mhe juma duni haji  kuhusu  makadirio na matumizi kwa mwaka wa fedha  2012 -2013

Alisema kuwa tamko hilo limetekeleza azma ya kiongozi mkuu wa serikali ,rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ya kuhakikisha kuwa akinamama wote wanapatiwa huduma ya uzazi bure .

Aidha alieleza kuwa mtu yeyote ambae atatolezwa pesa katika huduma za kizazi  ikiwemo  kujifungua kwa njia ya kawaida na upasuaji atoe taarifa kwa wizara husika ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria .

Waziri huyo alitoa pongezi kwa rais wa Zanzibar kwa uwamuzi wake wa busara  kuweza kufuta michango yote ya fedha kwa mama wajawazito .
Tamko hilo lilitolewa tarehe 9/05/2012 lenye lengo la kuwapunguzia makali ya maisha mama wajawazito, kupunguza vifo vya akinamama na watoto pamoja na kutekeleza malengo ya millenia
Aidha alisema kwamba katika kutekeleza mikakati wa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa akinamama huduma za kujifungua zinaendelea kuimarishwa katika hospitali zote za uzazi .
Amefahamisha kuwa hadi hufikia mwezi machi 2012 waliweza kupokea wajawazito waliolazwa katika hospitali ya idara ya tiba kwa unguja na pemba ni 8090kati ya wajawazito 6,075 walijifungua kwa njia ya kawaida na 395 walijifungua kwa njia ya upasuaji na akinamama 18 walifariki dunia na jumla ya watoto 6,528 walizaliwa katika kipindi hicho.

No comments:

Post a Comment