MAKAMU
WA RAIS WA NCHINI AFRIKA KUSINI,KGALEMA MOTLANTHE ( KATIKATI)
AKIANGALIA MOJA YA KABURI LA MPIGANIA UHURU WA ANC , ENEO LA
MAZIMBU,MJINI MOROGORO.
Makamu
wa Rais wa Afrika ya Kusini, Kgalema Motlanthe, Julai 9, mwaka huu
alifanya ziara ya siku moja Mjini Morogoro, ililiyokuwa mahusisi kwa
ajili ya kutembelea eneo la Mazimbu, ilikuwa kambi ya wapingania uhuru
wa Chama cha ANC.
Ziara
hiyo ilikuwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 20 tangu harakati za
ukombozi wa Afrika Kusini zilipomalizika ,katika Kambi hiyo , ANC
iliacha majengo na vitu mbalimbali vilivyokabishiwa Serikali ya
Tanzania, pia yapo makaburi kadhaa walimozikwa mashujaa hao, ambapo
Makamu huyo wa Rais aliweza kuzuru na kuweka shada la maua katika
mnara wa kumbukumbu ya wapigania uhuru hao pamoja na kupanda mti.
Kabla
ya kufanya shughuli hiyo,alipata fursa ya kutembezwa maneo mbalimbali
yakiwemo majengo yaliyokuwa yakitumiwa na wapigania uhuru hao, ikiwemo
Shule ya Msingi na Awali, Shamba la Mifuko, Kiwanda cha samani pamoja
na Hospitali .
MAKAMU
WA RAIS WA AFRIKA YA KUSINI AKITOA HESHIMA BAADA YA KUWEKA SHADA LA
MAUA KWENYE MOJA YA KABURI LA MPIGANIA UHURU WA ANC , ENEO LA
MAZIMBU,MJINI MOROGORO.
MAKAMU
WA RAIS WA AFRIKA KUSINI , KGALEMA MOTLANTHE, AKIPANDA MTI ENEO LA
MAKABURI YA WAPIGANIA UHURU WA ANC , MAZIMBU, MJINI MOROGORO.
MAKAMU
WA RAIS WA AFRIKA KUSINI AKITOKA KUTEMBELEA HOSPITALI YA MAZIMBU
AMBAYO ILIKUWA IKITUMIWA NA WAPIGANIA UHURU WA ANC, AMBAPO KWA SASA
IMEKARABATIWA NA KUONGEZWA MAJENGO MAPYA.
BAADHI YA RAIA WA AFRIKA KUSINI WALIOAMBATANA NA MAKAMU WA RAIS WA NCHI HIYO HAPA NCHINI.
BURUDANI
KWA MGENI RASMI,MAKAMU WA RAIS WA AFRIKA KUSINI ALIPOTEMBELEA SHULE YA
MSINGI CHIEF ALBERT LUTHULI, MAZIMBU MJINI MOROGORO.
No comments:
Post a Comment