Huu
ni mwaka ambao mkoa wa Kigoma utaongelewa sana kwenye burudani. Hongera
nyingi ziende kwa yule aliyekuja na wazo hili lenye thamani ambalo
limeunyanyua mkoa wa Kigoma katika kipindi kifupi mno.
Tangu
itoke Leka Dutigite, Kigoma imejipatia sifa kubwa kwa kujulikana
miongoni mwa wasanii waliojuu kwenye muziki wa kizazi kipya nchini kuwa
wanatokea huko. Ukizungumzia Diamond Platnumz na ukaona jinsi kijana
alivyofanikiwa mpaka kupiga show Big Brother, ni halali uheshimu mkoa
ulio asili yake, Kigoma. Tunafahamu kimaendeleo Kigoma ni miongoni mwa
mikoa iliyonyuma kwa Tanzania. Wanapaita ‘Kigoma mwisho wa reli’.
Jitihada hizi za mbunge wa Kigoma kaskazini, Mheshima Zitto Kabwe kuwapa
support wasanii wenye asili ya Kigoma, sasa zimegeuka mfano wa kuigwa. Tangu
wimbo ‘Leka Dutigite’, neno la kiha lenye maana ya Acha Tujidai, Kigoma
umekuwa ni mkoa unaojadiliwa sana na wapenzi wa burudani mitaani na
kwenye mitandao ya kijamii. Na hapo ndo utakapogundua kuwa Tanzania
hakuna ukabila. Watu wa mikoa mingine wameupenda wimbo huu na
kuwapongeza wasanii hao. Ni wimbo uliofanywa na masupastaa haswaa wa
Tanzania. Diamond, Peter Msechu,Ommy Dimpoz, Baba Levo, Banana Zorro,
Chege, Mwasiti, Linex, Queen Darling, Rachel na wengine wasanii waliojuu
sana nchini. Ni movement ambayo ikiwa nyuma ya mbunge mwenye kipaji cha
uongozi, Mhe. Zitto, inayoweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye mkoa
huo, kiuchumi na kisiasa. Ni muungano unaoweza kupeleka maendeleo
makubwa kwa kutumia mwavuli wa burudani. Ni movement ambayo itawaamsha
wasanii wengine na hata watu wa kawaida kuthamini asili yao. Wanasema
mtu asiyekuwa na kwao ni sawa na mtumwa. Itawaamsha wasanii waliopo Dar
es Salaamn(kitovu cha tasnia ya burudani nchini) kujivunia mkoa ama hata
kijiji anachotokea. Chema vizuri kuigwa. Mikoa mingine haitakuwa na
hasara ikifanya hivyo pia. Uzuri wa muungano kama huu, huchangia kukua
kwa sanaa kwenye mkoa husika. Tangu Leka Dutigite itoke, kuna wasanii
wengi wachanga wa mkoani Kigoma waliopata morali ya kuongeza juhudi
zaidi kimuziki ili wafanikiwe na hatimaye kupewa heshima kama hiyo ya
kujiunga na wakali wa mkoa huo. Japo baadhi yao kama wanavyosema kuwa
Kigoma ni asili yao tu lakini hawakukulia huko, asili ipo pale pale na
ni jambo la msingi kuutangaza. Baada ya kitendo hicho, leo hii watu
wengi wametamani wasanii wa mikoa yao wafanye kitu kama hicho pia. Huo
ni wivu wa maendeleo kama asemavyo Monty Khatau Ezel, “Nimevutiwa na
hiyo kitu, natamani ningekuwa natokea Kigoma,nina ugonjwa wa wivu wa
maendeleo,najivunia kutokea kusini,LINDI wajiandae mafanikio yanawajia.”
Ibrahim Athumani Masokola naye anasema, “Nahisi katika mambo ya kuiga
kwa baadhi ya watu kama waheshimiwa ni pamoja na hili analofanya mhe
Zitto kwani ni njia mojawapo ya kuwafikia wananchi kwa urahisi HONGERENI
SANA WOTE mlohusika kwa namna moja au nyingine.” Naye Zulu Agrey Mnkeni
anasema, “Natamani nami ningekuwa wa KIGOMA ila ndo bahati mbaya natoka
KILIMANJARO naogopa kuitwa MKABILA.” Kitendo hicho cha Mheshimiwa Zitto
kuungana na wasanii ili kuutangaza mkoa wa Kigoma,kinamweka karibu
zaidi na vijana waliowengi nchini na kumsafishia njia yake kwa mambo
makubwa zaidi katika career yake kama mwanasiasa. Hongereni Kigoma All
Stars!
No comments:
Post a Comment