Mwili wa Donald Mathew ‘Dunga’ ukiondolewa mtini.
ASKARI
jasiri aliyejizolea sifa mkoani hapa kwa kitendo chake cha kuwataja
hadharani baadhi ya askari wenzake akiwashutumu kwa tuhuma mbalimbali
zikiwemo za kushirikiana na majambazi kufanya uharifu, Donald Julius
Mathew, mwenye namba ya jeshi la polisi F3276 amekufa akidaiwa
kujinyonga.
Mwili
ya afande huyo ambaye ni maarufu mkoani hapa kwa jina la Dunga umekutwa
ukiningin'ia juu ya mti eneo la Daraja la Shani ambalo liko katikati ya
Mji wa Morogoro.
Dunga aliwalipua maafande zaidi ya sita ambao walihamishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema na yeye kuhamishwa mkoa wa Singida.
Hata hivyo, Dunga aligomea uhamisho huo akipinga watuhumiwa kutochukuliwa hatua.
Sababu alizotoa Dunga zinaelezwa katika barua aliyomwandikia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi aliyoitoa kwa mtandao huu na ambayo tunaichapisha.

NA KAPINGAZ BLOG
No comments:
Post a Comment