Pages

Tuesday, August 28, 2012

CHADEMA KUGARAMIA MAZISHI YA MTU ALIYEUWAWA KATIKA MAANDAMANO JANA MKOANI MOROGORO




 Katibu mkuuwa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Dr Slaa akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa  mount uluguru mkoa wa morogoro..



Baadhi ya viongozi waandamizi wa chadema walioambatana na katibu mkuu wa chadema kutoka kushoto aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la igunga ndugu joseph kashindye, katikati mkurugenzi wa haki na sheria wa chama hicho na mbunge wa singida mashariki mh Tundu Lissu, Kulia mkurugenzi wa operation sangara ndugu Benson kigaiya.
Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wamesema watagaramia mazishi ya kijana ally zona mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa morogoro aliyefariki jana katika maandamano ya chama cha demokrasia na maendeleo chadema kwa kupigwa risasi kichwani,
Hayo yamesemwa na katibu chama hicho dr Slaa wakatia akiongea nawaandishi wa habari leo mjini morogoro.Chadema wamesema wapo tayari kugaramia gharama zote za mazishi ya kijana huyo  mkazi wa kihonda magorofani mwenyeji wa wa mkoa wa Tanga aliyekuwa anajishugulisha nashuguliza kuuza magazeti katika kituo kikuu cha mabasi msamvu mkoani morogoro..

No comments:

Post a Comment