Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, August 25, 2012

Gambia yaanza tena kunyonga wafungwa



Rais wa Gambia, Yahya Jamme
Shirika la kimataifa la kutetea haki za kibinaadamu, Amnesty International, linasema limeambiwa kwamba Gambia imewanyonga wafungwa tisa kati ya 47 ambao wamehukumiwa kifo.
Tumepata taarifa za kuaminika kuwa watu 9 walinyongwa jana usiku.Msemaji wa Amnesty, Lisa Sherman Nichols, alisema kwamba wafungwa hao ni wa mwanzo kunyongwa nchini Gambia kwa miaka 29, na inasemekana alikuwako mwanamke kati yao, na wananchi watatu wa Senegal.
Nimezungumza na baadhi ya jamaa zao, ambao bila ya shaka wako kwenye majonzi, na wametuomba tuchukue hatua.
Wamegusia kuwa kuna wengine watanyongwa leo usiku.
Tunajaribu kuzitawanya habari hizi ulimwenguni na serikali ya Gambia inafaa kujua kuwa macho ya ulimwengu na serikali za nchi za nje yameelekezwa juu ya nchi hiyo."
Hapo awali, shirika la raia la nchi hiyo lilimlaumu rais wa Gambia, Yahya Jammeh, na lilisema kwamba wengi waliohukumiwa kifo ni wafungwa wa kisiasa.

No comments:

Post a Comment