Pages

Saturday, August 11, 2012

HALI YA UJANGILI KATIKA HIFADHI ZA TAIFA NI MBAYA


Mahmoud  Ahmad Arusha

Imeelezwa kuwa hali ya ujangili kwenye hifadhi za taifa na mapori ya akiba hapa nchini ni mbaya na ya kutisha kwani taarifa zinaonyesha kuwa mwaka 1989-2010 robo ya meno ya tembo yaliyokamatwa duniani kote yanatoka Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu wakati akiongea na vyombo vya habari kwenye hotel ya Mount Meru jijini hapa na kubainisha kuwa taarifa zinaonyesha42% ya tembo katika Selous Game Reserve na hifadhi ya taifa mikumi wametoweka katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Nyalandu alisema kuwa hiyo ni sawa na tembo zaidi ya 31,348 sawa na asilimia 42 na kuwa kumekuwepo na mtandao wa kimataifa wa(Sophisticated International Criminal Syndicate)unafanyakazi hapa nchini na kumekuwa na uchimbaji  mdogo wa madini kwenye mbuga za Serengeti kunakofanywa kinyume na sheria.

“Nimepata taarifa hizi za kushtusha kutoka wizara ya nishati na madini kwamba kuna shughuli za uchimbaji zinazoendelea kwenye mbuga za hifadhi hizi na wizara hiyo imenieleza kwamba haijatoa leseni ya uchimbaji ,utafiti wa madini kwenye hifadhi ya Serengeti hivyo wanaofanya uharamia huu ni kwa matakwa yao tena kinyume cha sheria”alisema Nyalandu
.
Taarifa hizi zinatishia hali ya usalama wa tishio dhidi ya uhifadhi itakubukwa kuwa hifadhi ya Serengeti ni sehemu ya urithi wetu na dunia unaosimamiwa na wold Heritage Committee chini ya (UNESCO) na serekali ya Tanzania inayo dhamana ya kuulinda urithi huu kwa niaba ya watanzania na dunia.

Nyalandu akatoa agizo kwa bodi ya wadhamini ya mamlaka za hifadhi za taifa(TANAPA)itoe maelezo ya kina kuwepo watumishi wa ndani ya mamlaka na hifadhi wanaosadikiwa kushirikiana na majangili pamoja na maharamia kuendesha shughuli hizi zinazo hatarisha hifadhi zetu na heshima ya Serengeti.

Alisema kuwa kuna taarifa hali tete za  kuongezeka vitendo vya kijangili kuwepo shughuli za uchimbaji wa madini katika hifadhi za Serengeti.

No comments:

Post a Comment