Pages

Wednesday, August 8, 2012

KAMPUNI YA STEPS NA WASANII WA BONGO MOVIE WAKAMATA NAKALA FEKI ZA KAZI ZAO



 Gari lenye namba za T 608 BWD lililokamatwa na kazi mbalimbali za wasanii zikiwemo zinazosambazwa na Kampuni ya Steps ya jijini Dar es salaam linalofanya kazi na wasanii hao
 Moja ya gari lililokuwa limejaa kazi za wasanii mbalimbali nchini zinazouzwa kiholera baada ya kurudufu kinyume na sheria na kukosesha wasanii mapato mazuri.

 BAADHI YA KAZI FEKI ZA WASANII ZILIZOKAMATWA LEO
 MSANII MOHAMED NICE 'MTUNISI' AKIZUNGUMZA JINSI WALIVYOKAMATA MZIGO FEKI WA KAZI ZA WASANII MBALIMBALI KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTATAINMET YA JIJINI DAR ES SALAAM INAYOSAMBAZA KAZI ZA WASANII NCHINI
 MSANII MOHAMED 'NICE' AKILIA KWA UCHUNGU BAADA YA KUKUTA KAZI ZAO ZILIZOKUWA ZIKIUZWA KATIKA MOJA YA DUKA MTAA WA MAGILA NA LIKOMA LEO
 MTUUMIWA WA KURUDUFU KAZI ZA WASANII AKIWA CHINI YA ULINZI BAADA YA KUKAMATWA
 MSANII WWA MZIKI WA TAARABU,MZEE YUSUFU KUSHOTO AKIANGALIA MOJA YA KAZI YAKE ILIYOKUWA FEKI ZILIZOKAMATWA NA WASANII WENYEWE KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTANTAINMENT YA JIJINI DAR ES SALAAM
 WASANII MZEE YUSUFU KUSHOTO NA MOHAMED NICE WAKIWA KATIKA DUKA LILILOKAMATWA KWA KUUZA KAZI FEKI ZA WASANII MSAKO HUO ULIWASHILIKISHA KAMPUNI YA STEPS ENTATAINMENT PAMOJA NA WASANII WENYEWE
 MSANII KAPTEN RADO AKIKAGUA KAZI ZAKE MPYA AMBAPO KAZI YAKE MPYA IJULIKANAYO KAMA 'HATIHANI' ILIYOINGIA MTAANI LEO ILIKUWA IMESHA CHAKACHULIWA NA KUINGIZWA SOKONI
 Msanii wa filamu nchini Mohamed Nice 'Mtunisi' kushoto na Jacob Stevin 'JB' wakiwa katika duka ambalo lilikuwa linauza kazi zao ambazo ni feki ambapo walikamatwa kwa kushilikiana na Kampuni ya usambazaji ya Steps Entantainment ya jijini Dar es salaam
 MSANII MOHAMED NICE 'MTUNISI'  KUSHOTO AKITOA MAELEZO MBALIMBALI KWA MAOFISA USALAMA WALIOFIKA KATIKA UKAMATAJI WA KAZI FEKI ZA WASANII
 Baazi ya wasanii pamoja na askari polis wakiwa wamerizingira duka lililokuwa linauza kazi za wasanii feki
 BAADHI YA WANANCHI WAKISHUDIA TUKIO HILO
 BAADHI YA MIZIGO YA DVD MPYA KABISA ZILIZO FEKI ZIKIWA ZIMEKAMATWA LEO
Baazi ya watu wakiwa wamezagaa kushudia ukamatwaji wa kazi za wasanii mtaa wa Magili na Likoma Dar es salaam leo
--
 KAMPUNI ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam inayosambaza kazi za wasanii kwa kushirikiana na wasanii wamekamata kazi mbalimbali za wasanii hawo zinazorudifiwa kinyume na taratibu na kutofaidika kwa wasanii wanaotoa kazi hizo

Msemaji wa Kampuni ya Steps  Kambarage Ignatios amesema kuwa ukamataji huo si wa zimamoto watahakikisha wanashilikiana na wasanii wenyewe kukamata kazi zao mana wasanii wengi wanadai kuwa kazi zao zinatoka sana kumbe zinachakachuliwa na kuwapa faida watu ambao wanakaa tu na kusubili kazi za wasanii ameiomba serekali kuchukua atua kali ili iwe fundisho kwa watu wanaorudufu na kunyonya kazi za wasanii hawo

Na mmoja ya wasanii waliojitokeza katika kamatakamata hiyo iliyofanyika makutano ya mtaa wa Magila na Likoma Kariakoo, Msanii Mohamedi Nice 'Mtunisi' amesema watu hawa wana akili za ziada kwani katika kava ya mbele wanaweka stika yetu halali na dvd ndio inakuwa imechakachuliwa akiangua kilio na kusema wasanii  wakifa wanakufa masikini kumbe ni watu wachache ndio wamekuwa wakinufaika na kazi zao bila kushiriki chochote

Baadhi ya wasanii walioshiliki katika kamata kamata hiyo ni pamoja na Jacobo Stevin 'JB' Mzee Yusuph wa kundi la Taarabu la Jahazi Simoni Mwapagata (Rado) Mussa Msuba wa iliyokuwa Segere Orginal Seles Mapunda ,Mohamed Nice 'Mtunisi' na wengine wengi wasanii hawo wameungana pamoja kwa ajili ya kutetea kazi zao ili zisirudufiwe kiolela na kuiomba serekali  kupitisha sheria kali kwa mtu anaekamatwa na kazi kama hizo zilizokamatwa

No comments:

Post a Comment