Majambazi
waliokuwa wamejihami wameshambulia kambi ya kijeshi mjini Abidjan, mji
mkuu wa Ivory Coast na kuwaua takriban wanajeshi sita.
Wenyeji
walielezea kusikia milio ya risasi usiku kucha katika mtaa wa Riviera.
Idadi kubwa ya wanajeshi wakiwemo walinzi wa amani wa umoja wamataifa,
wamepelekwa katika eneo hilo ingawa sasa maafisa wakuu wanasema kuwa
hali imeweza kudhibitiwa.
Mji
huo ulishuhudia mapambano makali, mwaka jana wakati wa mvutano wa
kisiasa ambao ulitokea baada ya matokeo ya uchaguzi ambayo yalizua utata
mkubwa.
Mnamo
siku ya Jumapili, wapiganaji waliokuwa wamejihami walishambulia kizuizi
cha jeshi barabarani katika eneo la Yopougon mashariki mwa Ivory Coast
pamoja na kituo cha polisi na kuwaua wanajeshi watano katika kambi ndogo
ya kijeshi mjini Abidjan.
Wapiganaji hao walivalia sare za kijeshi na kutumia silaha nzito nzito japo hawakuweza kutambuliwa.
No comments:
Post a Comment