Pages

Friday, August 10, 2012

MASTAA WAMVUA NGUA HEMED


Hemed Suleiman a.k.a PHD.
Na Hamida Hassan
BAADA ya hivi karibuni msanii wa filamu, Hemed Suleiman a.k.a PHD kutamba kuwa ametembea na mastaa 32, huku akijinadi kutotumia kondom wakati mwingine, baadhi ya mademu mastaa ‘wamemvua nguo’, Ijumaa linakuhabarisha.
Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti mastaa hao wameonesha kukereka na maneno hayo na kusema alichokifanya Hemed kimemchafua mbele ya jamii.
“Kwa kweli amejishushia heshima sana mbele ya jamii, wala hawezi kusifiwa kwa hilo kwani ni la kijinga,” alisema staa mmoja mwenye jina kubwa ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kuepuka bifu.
Aunt Ezekiel
“Akili zake si mzuri, kujisifia haimaanishi ni rijali kuliko wengine, ni upuuzi na ni hatari hasa ukichukulia kwamba kuna gonjwa la Ukimwi.”
Nisha
“Kusema hivyo atakuwa ameamua mwenyewe ila ametudhalilisha kwani ni bora kuwataja kuliko kuishia kutaja idadi kubwa, ila mimi simo.”
Thea
“Ni kukosa busara, anaonekana anatafuta umaarufu, tu bora angetaja hao aliotembea nao.”
Jack wa Chuz
“Hemed si taipu yangu kwa hiyo hata kwenye hiyo listi yake simo ila ningemuona mjanja kama angewataja.”
Jack Dustan
“Alichokifanya wala si kizuri, eti katembea na mastaa 32, ili iweje sasa? Atakuwa amekosa la kufanya ndo’ maana ....”
Rose Ndauka
“Kila mtu ana akili yake, siwezi kusema amekosea kutoa maneno hayo kwani akili yake ndiyo imemtuna na kila mtu ana maisha yake, ninachoshukuru mimi simo.”
Hivi karibuni Hemed alitoa maneno yaliyowashangaza wengi pale alipokuwa akifanya mahojiano na Blog ya Mvutokwanza na kuulizwa idadi ya mastaa aliotembea nao ambapo alisema:
“Unauliza kengele kanisani? Unadhani kwa nini naitwa Hemed PHD? Nina taaluma ya kucheza na mioyo ya mabinti hawa wa Kibongo ila tatizo hawanivutii, huwa napita tu. Mpaka sasa nishawapitia mastaa 32....”
SOURCE GLOBAL PUBLISHER

No comments:

Post a Comment