Siku Mwakalebela na mkewe walipopandishwa kizimbani na TAKUKURU Iringa
Siku Mungai alipopandishwa kizimbani na TAKUKURU Iringa
Siku Mungai alipopandishwa kizimbani na TAKUKURU Iringa
TAASISI ya kuzuaia na kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Iringa yazidi kumng’ang’ania aliyekuwa waziri wa wizara mbali mbali katika awamu mbali mblia katika serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mufindi Kaskazin Joseph Mungai kwa lengo
la kumfikisha mahakamani ili kujibu mashitaka ya kujihusisha na rushwa
katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM mwaka 2010.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mjini Iringa kaimu mkuu wa
Takukuru mkoani hapa Stephen Mafipa amesema taasisi hiyo inamtafuta
mheshimiwa mungai ili kumfikisha mahakamani kujibu mashitaka hayo baada
ya mahakama kuu kanda ya Iringa kupitia kwa jaji kiongozi wa mahakama
hiyo sekieti kihio kutupilia mbali rufaa yake.
katika
rufaa yake aliyokata kupitia kwa mawakili wake wawili basiri mkwata na
Alex Mgongolwa Mungai aliiomba mahama hiyo kutupilia mbali uamuzi wa
mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa kupitia kwa mheshimiwa marry
senapee tarehe 31 january 2011 ambapo alitupilia mbali hati yamashitaka
ya rushwa yaliyokuwayakimkabli mheshimiwa mungai na kuamuru upande wa
mashitaka kufanyia marekebisho hati hiyo na kumfikisha mahakamani
mtuhumiwa.
katika
rufaa yake mh.mungai aliiomba mahakama hiyo kutupilia mbali uamuzi wa
mahakama ya hakimu mkazi na kisha kutolea maamuzi hoja nyingine ambazo
hazikutolewa maamuzi na mahakama hiyo ya hakimu mkazi ambapo katika
makosa yote 15 ya kutoa rushwa ambayo mungai alikuwa akishitakiwa nayo
yalikuwa siyo makosa ya jinai kwa kukosa maneno muhimu kisheria kama
inavyotakiwa katika kifungu cha 15 (1)(b) cha sheria ya kuzuia na
kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
katika
hoja ya pili bwana mafipa amefafanua kuwa kifungu cha 21(1) (a) na
kifungu cha 24 (8) cha sheria ya gharama za uchaguzi,sheria namba 6 ya
mwaka 2010.ambacho mheshimiwa mungai na wenzake walishitakiwa nacho
kilikuwa hakitengenezi kosa la jinai kisheria .
Aidha taasisi hiyo inakusudia kumkamata na kumfikisha mahakamani
aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha soka nchiniTFF Fredrick Mwakalebela
ili kujibu kesi kama hiyo ya rushwa ya uchaguzi mwaka 2010 baada ya
rufaa yake inayofanana na ya mheshimiwa mungai kutupiliwambali na
mahakama kuu kanda ya Iringa siku chache zilizopita
Mungai
na mwakalebela walikuwa wagombea ubunge katika majimbo ya mufindi
kaskazini na Iringa mjini ambapo wote wanatuhumiwa kuwa walitumia
ushawishi wa rushwa kwa wapiga kura katika mchakato wa kura za maoni
ndani ya chama cha mapinduzi ccm.
No comments:
Post a Comment