Mwanamke
mmoja nchini Sudan aliyepatikana na hatia ya kufanya uzinzi anakabiliwa
na adhabu ya kupigwa mawe hadi kufa iwapo mamlaka za nchi hizo
hazitampa rufaa dakika za mwisho.
Wanaharakati
wamesema mwanamke huyo Laila Ibrahim Issa Jamool mwenye umri wa miaka
23 amekuwa chini ya ulinzi akiwa amefungiwa katika bomba chuma pamoja na
mwanae mwenye umri wa miezi 6 baada ya kuhukumiwa na mahakama katika
mji mkuu wa Khartoum mnamo Julai 10.
Mwezi
uliopita rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan alisema nchi hiyo
itaridhia kwa aslimia 100 Katiba ya Kiislam baada ya kutengana na taifa
lisilo la kiislam la Sudan Kusini mwaka mmoja uliopita.
Mume wa mama huyo alimtuhumu mkewe kwa kufanya zinaa, ambapo ni kinyume kwa mujibu wa sheria za adhabu za Sudan za mwaka 1991.
Hukumu
hiyo ya kifo kwa kupigwa mawe ni ya pili kupitishwa nchini Sudan kwa
kosa kama hilo katika kipindi cha miezi michache iliyopita.
No comments:
Post a Comment