Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, August 24, 2012

Rada ya Chenge yaanza kufanya kazi



Fidelis Butahe na Zaina Malongo WAZIRI wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe amesema rada ya kuongozea ndege kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere iliyokuwa imeharibika tangu Agosti 3 mwaka huu, imetengenezwa na  kuanza kufanya kazi juzi saa 2:45 usiku. 
Agosti 17 mwaka huu, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ilisema rada hiyo iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania kutoka Kampuni ya Silaha ya BAE Systems ya Uingereza ilikuwa imeharibika, ikiwa ni siku moja tangu  gazeti dada la Mwananchi (The Citizen) kuripoti  juu ya kuharibika kwa rada hiyo, hali iliyoelezwa kuwa itahatarisha usafiri wa anga nchini.  Alifafanua kwamba kifaa kilichokuwa kinasumbua kimeondolewa na kuwekwa kingine na kuongeza kuwa  wameagiza vifaa vingine vya ziada.

No comments:

Post a Comment