RUFAA
ya kupinga kuvuliwa ubunge ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha
Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), imepangwa kusikilizwa Septemba 20, mwaka
huu, mbele ya majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa; Natalia Kimaro,
Mbarouk Salim Mbarouk na Salmu Massati.
Kwa
mujibu taarifa za kikao cha Mahakama ya Rufaa cha Arusha, rufaa hiyo
iliyofunguliwa na Lema akipinga uamuzi uliotengua ubunge wake kufuatia
shauri lililofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, inatarajiwa
kusikilizwa kwa siku moja ambapo baada ya hapo itapangwa tarehe kwa
ajili ya kutoa uamuzi.
Awali,
Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro, aliwasilisha kwenye
mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.
Kwenye
baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi
wa Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa
mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.
No comments:
Post a Comment