Pages

Thursday, August 30, 2012

SAMUEL ETO'O AKATAA KUICHEZEA CAMEROON BAADA YA KUTOKA KWENYE KIFUNGO CHA MIEZI NANE

Samuel Eto'o  amekataa kuichezea Cameroon katika kutekeleza mgomo wake dhidi ya kile alichokiita "mpangilio mbovu na mazingira yasioeleweka" katika kikosi cha timu ya taifa.

Mshambuliaji huyo alikuwa kwenye kikosi cha Cameroon kwa ajili ya kupambana na Carpe Verde katika michuano ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika mwezi September baada ya kumaliza adhabu yake kufungiwa miezi nane.

Lakini Eto'o alisema kwenye barua yake aliyoiandikia shirikisho la soka la Cameroon hatoweza kurejea kwenye timu ya taifa kwa sababu matatizo yote yaliyomfanya akafungiwa bado hajatafutiwa ufumbuzi.

Eto'o, ambaye ameshaichezea nchi yake mechi 109 na kufunga mabao 54, alifungiwa kutokana na kuongoza mgomo wa wachezaji baada ya kutolipwa posho zao.

Shirikisho la soka la Cameroon liliamuarifu Eto'o na mwanasheria wake pamoja na timu yake ya Anzhi Makhachkala kwamba kifungo chake kimeisha mapema wiki hii.

Na kocha Denis Lavagne akamchagua Eto'o katika kikosi chake cha wachezaji  23 kwa ajili ya kucheza dhidi ya Cape Verde tarehe 8 mwezi ujao kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya kufuzu kushiriki AFCON 2013.

Lakini nahodha wa Cameroon bado amekosa furaha dhidi ya masuala ya uongozi mbovu kwenye timu ya taifa na suala lao la kuwapandisha wachezaji ndege daraja la pili tena kwenye safari ndefu - na kutokana na sababu hizo mshambuliaji huyo wa zamani wa Barca amejiondoa kwenye timu ya taifa.

"Timu yetu ya taifa inaendelea kupotea kutokana na mazingira mabovu na mpangilio usioleweka kwenye timu ya taifa - vitu ambavyo haviendi sawa na michezo ya kisasa," aliandika Eto'o katika barua yake kwenye kwa CFF ambayo pia imewekwa kwenye mtando wake.

"Nina mashaka washabiki wa timu ya taifa wataelewa hatua yangu hii ambayo mlengo wake mkuu ni kubadilisha mambo yote ya hovyo kwenye timu ya taifa na kuyafanya kuwa bora.

"Timu ni taasisi yenye heshima ambayo imechangia sana mafanikio ya nchi" - alimaliza Etoo.

No comments:

Post a Comment