Pages

Wednesday, August 22, 2012

VURUGU ZAZUKA KARIAKOO, NI UGOMVI WA KUGOMBEA NYUMBA, FFU WAMALIZA KAZI



Askari wa FFU wakiwa wameimarisha ulizi baada ya vurugu kuzuka katika  mtaa wa Kongo Kariakoo jijini Dar es salaam leo jioni juu kutokana na wakazi wa mtaa huo  kugombania nyumba baina ya mpangaji na mwenye nyumba,Askari walifika eneo la tukio na kuimarisha ulinzi hata hivyo walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi   kuwatawanya watu walioko katika maeneo hayo wakishiriki katika vurugu
Nyumba ambayo inasadikiwa kuleta vurugu hizo ikiwa inavunjwa na vijana wa kampuni ya Yono Actin Mart katika  mtaa wa Kongo Kariakoo jijini Dar es salaam
Wakazi wa eneo hilo wakiwa mamedhibitiwa wasiingie katika eneo la tukio
RISASI na mabomu ya kutoa machozi leo vimerindima maeneo ya Kariakoo baada ya mtu mmoja kuvamia nyumba kwa zaidi ya miaka 40 akidai kuwa ni yake.
Hali hiyo imekuja baada mmiliki halali wa nyumba hiyo, Samiri Said kushinda kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo mahakama ili mtaka mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Shaban Hassan kuondoka katika nyumba hiyo.
Akizungumza na full.blogspot jijini Dar es Salaam jana kiongozi wa Kampuni ya Udalali ya Yono, Isaac Nguku alisema walifika eneo hilo kwa amri ya Mahakama kwa lengo la kukabidhi nyumba hiyo kwa Said.
Alisema hata hivyo, walipofika katika eneo hilo majira ya saa 5:00 asubuhi walikuta kundi la vijana ambao inasadikika kuwa waliandaliwa na Hassan kwa ajili ya kukwamisha zoezi hilo.
Nguku alisema baada ya kuona hali hiyo waliamua kuomba msaada kutoka polisi ambapo walifika na kuanza kuwatawanya vijana hao.
“Vijana hao hawakuridhika ndipo wakaanza kuturushia mawe kutoaka kona zote walizokuwa wamejipanga kitendo hicho kilisababisha askari kufyatua risasi za moto juu huku wakipiga mabomu ya machozi na kuwatawanya mbali”alisema Nguku.
Baada ya vijana hao kutawanyika mitaa minne inayozunguuka nyumba hiyo ilifungwa, mitaa hiyo ni pamoja na Kongo, Mkunguni, Tandamti na Mchichi.
Naye mmiliki wa nyumba hiyo, Said alisema wavamizi hao walipanga katika nyumbani hiyo tangu mwaka 1972 ambapo baada ya hapo wakajitengezea hati bandia kwa lengo la kumdhulumu mama yake mzazi.
Alisema kitendo hicho kiliwafanya wafikishe kesi hiyo mahakamani ambako waliwakilisha hati zao ambazo zimewafanya washinde kesi hiyo, mvamizi huyo  kuamriwa aondoke kitendo alichokipinga huku akikata rufaa za mara kwa mara lakini hata hivyo akawa anashindwa mara zote.
Nyumba hiyo inayogombewa iko mtaa wa Karikoo kitalu namba 86, hata hivyo wakati zoezi hilo likiendelea mvamizi huyo yuko ndani kwa ajili ya kutumikia kifungo cha siku 21.
Hadi fullshangwe.blogspot ikiondoka katika eneo la tukio lililokuwa limesambaa mawe yaliyokuwa yakirushwa na kikundi hicho kinachomuunga mkono mvamizi huyo, vijana zaidi nne walikuwa wamekamatwa na polisi huku mmoja wao akiwa ameumia usoni kutokana na purukushani na  polisi.

No comments:

Post a Comment