Pages

Sunday, August 5, 2012

Wananchi Wapata Kiwewe juu ya ugonjwa wa ebola!!!




WANANCHI waishio mpakani mwa Tanzania na Uganda wameingia na hofu baada ya kugundulika kuwa ugonjwa hatari wa Ebola imeingia nchini.

Watu wengi mkoani hapa kuanzia juzi walionekana kuingiwa na wasiwasi baada ya taarifa kuzagaa kuwa mgonjwa mmoja amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Karagwe ya Nyakahanga, mkoani hapa.

Wengi walisikika wakishauri serikali za Uganda na Tanzania kushirikiana kudhibiti ugonjwa huo usizidi kusambaa zaidi.

Inaelezwa kuwa mgonjwa huyo aliingia nchini akitokea nchi ya Uganda na kwamba hivi sasa amelazwa katika Hospitali ya hiyo chini ya uangalizi maalumu wa madaktari.

Wananchi wazungumza
Wananchi hao walisema kuwa katika maeneo kama Mutukula ni vigumu sana kudhibiti mtu mwenye ugonjwa asiwaambukize wengine kutokana na mwingiliano mkubwa wa kibiashara uliopo.

Mkulima katika eneo hilo lililopo Wilaya ya Missenyi, Samihu Majidu alisema kuwa tangu walipotangaziwa kuchukua tahadhari, wanaishi kwa wasiwasi, wanaogopa kugusana na kushikana mikono.Naye, Sauda Hassan, Mtanzania anayefanya biashara katika eneo la Mutukula alisema

kuwa hata kama watakuwa makini kivipi, lakini bado vyombo vya usafiri ni tatizo kubwa linaloweza kueneza ugonjwa huo kwa kasi.
“Wenyewe mnaona hali ilivyo, watu wa Mbalala, Busia (Uganda) wako hapa, kama mtu ana ugonjwa utazuiwa vipi?” alihoji.

Aliongeza: “Wanakuja wamebanana kwenye magari wakati tunaambiwa msigusane, magari yanajaza sana abiria wengine wanasimama.”Sauda alisema: “Tunafanya biashara hapa, mteja anakuja anakupa hela unashika bila kinga yoyote kama mteja ana ugonjwa ukashika hela ambayo ina majimaji utaugua, Nadhani tununue mipira ya kuvaa mikononi wakati wa kufanya biashara maana tukisema tuache biashara uchumi utashuka.”

Alisema hata kama Serikali itafunga mpaka wa nchi hizo bado tatizo litakuwepo kutokana kuwepo kwa njia nyingi za panya.
 Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Nyakahanga, Dk Andrew Cesari alikiri kupokea mgonjwa mwenye dalili zinazowiana na za ugonjwa wa ebola.

Alisema mgonjwahuyo alipelekwa hospitalini hapo akitoka eneo la Kyerwa ambalo lipo mpakani na nchi hiyo ya Uganda.
Dk Cesari alisema kuwa mgonjwa huyo alikuwa ana homa kali, alivuja damu sehemu mbalimbali za mwili wake na kutaapika.
Daktari huyo alisema kwa mujibu wa maelezo ya ndugu zake, mgonjwa huyo alianza kupatiwa matibabu nyumbani kwao na alipoonekana kuzidiwa ikibidi wampeleke hospitalini hapo.

Alisema mgonjwa huyo alipokelewa katika chumba maalum na kupelekwa katika wodi ya magonjwa hatari ambapo ametengwa na anaendelea vizuri. “Damu sasa imesimama kutoka, ameacha kutapika, lakini bado hatujajiridhisha kama ugonjwa alio nao ni Ebola maana yapo magonjwa mengine yanayoweza kumfanya awe na dalili hizo,” alisema. 
Alisema dalili za awali za mgonjwa wa Ebola ni homa, uchovu wa viungo, mafua, koo kuwasha, kutapika na kuharisha.


No comments:

Post a Comment