Pages

Monday, August 20, 2012

YANGA YAICHAPA AFRICA LYON 4-0 UWANJA WA TAIFA



Mchezaji wa timu ya Yanga Oscar Joshua akikokota mpira kuelekea katika goli la Africa Lyon huku beki wa timu ya hiyo akijaribu kuufukuzia ili kuzuia katika mchezo wa kirafiki uliokutanisha timu hizo ambazo zote zinashiriki Ligi kuu ya Tanzania Bara, mchezo huo unafanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam tayari Yanga inaongoza goli 4-0 dhidi ya Africa Lyon mawili yakifungwa na Haruna Niyonzima na goli la tatu limefungwa na Frank Dumayohuku mchezaji Jerryson Tegete akimalizia kufunga goli la nne dakika 90
Mchezaji wa timu ya Yanga Khamis Kiiza akiwania mpira mbele ya golikipa wa timu ya Africa Lyon Juma Abdul mwenye namba 30 mgongoni wakati wa mchezo wao wa kirafiki kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kocha wa timu ya Africa Lyon Muargentina  Pablo  akionekana kulalamikia jambo kwenye benchi la ufundi la timu yake  wakati timu yake ilipokutana na timu ya Yanga katika mchezo wa kirafiki kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Kikosi cha timu ya Africa Lyon kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpambano huo kuanza.
Kikosi cha timu ya Yanga kikiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa Taifa kabla ya kuingia uwanjani.
na full shangwe

No comments:

Post a Comment