Watu 11
wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi haramu la Mombasa Republican
Council (MRC) wameuwawa katika eneo la msitu wa Bamba eneo la Kilifi
katika Mkoa wa Pwani.
Mkuu wa
Polisi eneo la Pwani ya Kenya Bwana Aggry Adoli amethibitisha tukio hilo
akisema kuwa wanakijiji waliwaona watu walioshukiwa kuwa wanachama wa
MRC wakiingia msituni na kuwafuata na kisha kuwaua baadhi ya watu
waliokuwa kwenye kundi hilo.Endelea kupitia audifacejackson blogspot.Eneo
la Pwani mwa Kenya limekuwa na migogoro ya kila aina kuanzia kwa
uhasama kati ya jamii hasimu zinazoishi pembezoni mwa mkoa
huo.Walikamatwa na silaha za kijadi kama vile panga na visu. Polisi
wanasema kuwa mmoja wao alikuwa mganga wa kienyeji
Polisi
wamekua wakilaumiwa kwa kukosa kudhibiti ulinzi mkoani humo hasa wakati
huu wa heka heka za maandalIzi ya uchaguzi utakaofanyika mwezi Machi
mwaka ujao.
Hata
hivyo bwana Adoli anasema kuwa utovu wa usalama sio kosa la polisi bali
ni kutokana na matatizo yanayokumba jamii za eneo hilo.
No comments:
Post a Comment