Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi amesema anapitia taasisi
zote zilizopo chini ya wizara yake ili kusikiliza mafanikio na kujua
matatizo yanazozikabili taasisi hizo ili kuweza kuboresha huduma
katika sekta ya afya nchini pamoja na kupanga mipango mizuri katika
kuendeleza taasisi hizo.
Dkt. Mwinyi amesema hayo leo kwenye ziara yake na kuzungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Chakula na Liche Tanzania (TFNC).
“Lazima
tujiulize uwepo wa taasisi hii,mwanzoni taasisi hii ilikuwa inajikita
na utapiamlo, kwa sasa kuna magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ,alitaja
mfano wa magonjwa haya ni moyo,kisukari na mengineyo magonjwa haya
mapambano yake ni kinga,na wataalamu wa kutoa kinga ni nyinyi,hivyo
masuala ya lishe ni muhimu kabla ya kuanza kuyatibu.
Aidha
Dkt. Mwinyi alisema wizara yake ina kila sababu ya kuyapa kipaumbele
masuala ya lishe nchini licha ya ufinyu wa bajeti wanayoipata, “ipo haja
ya kujipanga upya na kufanya kitu cha ziada ili kupunguza kiwango cha
utapiamlo nchini pamoja na upungufu wa wekundu wa damu kwa wanawake
wenye umri wa kuzaa ambapo inachangia vifo vya akina mama wajawazito nah
ii inachangia na akina mama wengi kutokuwa na elimu na mafunzo juu ya
lishe na hivyo nchi kuwa nyuma na kutofikia malengo ya millennia ya
kupunguza vifo vya akina mama wajawazito nchini.
Awali
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Benetict Jeje alisema
taasisi yake ina changamoto ya kuhakikisha kuwa huduma za lishe nchini
zinapanuka na kuwafikia wananchi wengi hasa waishio vijijini , hivyo
serikali kuamua kuajiri maafisa lishe katika halmashauri 106 kati ya
168 na mikoa 11 imefanya hivyo.
“Lishe
ni suala mtambuka na linalogusa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na
maendeleo ya nchi kwa ujumla,ushiriki wa sekta mbalimbali katika
kukabliana na changamoto za lishe nchini ni jambo lisiloepukika”alisema
Jeje.
Hata
hivyo alisema taasisi yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
zimechangia kupunguza kwa kiwango cha utapiamlo nchini kati ya mwaka
1999 na 2010.Asilimia 16 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano wana
uzito pungufu,asilimia 5 ni wakondefu na asilimia 42 wana udumavu na
upungufu wa damu unaathiri asilimia 69 ya watoto wakati upungufu wa
vitamin A ni asilimia 33.
No comments:
Post a Comment