Hii post inamuhusu aliekua mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambae alivuliwa ubunge na Mahakama.
Kuna
mambo mengi niliyotamani kumuuliza kabla ya kukutana nae ambayo hata
hivyo nilimuuliza na yote akayatolea ufafanuzi kwenye hiyo exclusive
interview.
Kuhusu
kupata vitisho, Lema amesema “kutishwa, kutukanwa ama watu kukufatilia
wengine kukutishia wengine kujifanya wanakuangalia kimpango, taarifa
hizo ni nyingi lakini hivyo sio vitu vya kunitisha wala sitembei na
mlinzi na siogopi nitaendelea kufanya kazi ya ukombozi kwa sababu kwanza
siwezi kuishi milele, kuna watu hawafanyi harakati za ukombozi lakini
wako wanakufa Muhimbili kwa magonjwa kama Malaria”
Kwenye
sentensi ya nyongeza naendelea kumkariri Lema akisema “mimi ni bora
nikapigwe risasi lakin mchungaji akija kusoma risala aseme marehemu
amekufa akipigania haki, kifo kwangu kimeshapoteza kumbukumbu na uoga
kwangu umeshapoteza kumbukumbu, siogopi kufa siogopi jela ila naogopa
kwenda jela kwa wizi wa kompyuta, Tv au kubaka mwanamke lakini siogopi
kwenda jela kwa kupigania haki za watu, wanaoleta vitisho
ninawakaribisha.. ni vingi na vingine tunavifanyia utafiti sisi wenyewe
tujue chanzo ni nini, hata muundo wa serikali ulivyo dhidi ya wapinzani
ni kitisho namba moja, kwamba wewe ni mbunge unafanya kazi na DC ama na
mkuu wa mkoa ambae ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya CCM”
Kauli
nyingine aliyoitoa Lema ni kuhusu kesi yake kwa sasa kwa kusema “sitaki
mahakama ya rufaa inipendelee sitakia hata kidogo, ikinipendelea
nitalia, nitaogopa nitasikitika nikijua nilifanya makosa ya kuua alafu
nikaachiwa huru, niko tayari kurudi kwenye uchaguzi na nitashinda kuliko
mbunge yeyote Afrika Mashariki kwa kura za kubeba na Canter ila
ninachotaka ni haki itendeke ila nimepata faraja kwamba anaeongoza kesi
yangu ni jaji mkuu wa Tanzania nikiamini atapitia vipengele vya kisheria
vizuri kabisa”
Pamoja
na hayo yote, Godbless Lema amesema hajawahi kujuta kuwa nje ya bunge
ila anajuta kwa nini Mahakama iliingiliwa na kumfanya ajue matokeo ya
kesi siku 14 kabla ambapo namkariri akisema “Halima Mdee alinipa matokeo
ya kesi mpaka kifungu kinachokwenda kunibana, Dr Slaa anaingia
mahakamani ananiamba mwanangu unakwenda mahakamani lakini hukumu yako
itakua hivi, ile kesi hukumu ilivuja kwa hiyo maana yake ilikua ni
mpango, ni kitu kimepangwa”
“Kilichoniumiza
sio mimi kutokua mbunge, ninaweza kuishi nje ya Ubunge ninaweza kuuza
mitumba, ninaweza kuwa dereva wa daladala, ninaweza kucheza soka..
ubunge kwangu sio ajira naweza kuishi maisha mazuri kuliko kuwa mbunge,
nimekua mfanyabiashara siku za nyuma sijakwenda Ulaya nikiwa mbunge,
nimekwenda ulaya kabla sijawa mbunge nimekwenda karibu nchi 16 za Ulaya
na nimefanya biashara lakini nilipopata ubunge nikasema nimepata nafasi
ya kutumikia watu”..SOURCE MILLADAYO
No comments:
Post a Comment