Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
Imeelezwa kuwa kila mwananchi ana
haki ya kujua kile ambacho anastahili kujua na anawajibu wa kuelezwa
hali halisi ya mambo yenye ukweli .
Kauli hiyo imeelezwa leo na
Mwenyekiti wa Hati Miliki Mariyam Hamdani wakati akifungua kongamano la
siku moja linalohusu siku ya kujua duniani huko katika ukumbi wa
Mazson Hoteli Zanzíbar .
Alisema kuwa mwananchi yoyote awe
mkubwa au mdogo anahaki ya kujua kila kitu ambacho anastahiki akijuwe
ili áweze kuwa muelewa zaidi wa mambo mbali mbali ya ndani na nje ya
nchi .
Aidha alisema kuwa siku ya kujua
duniani ni siku muhimu kwa kila binaadamu yeyote mwenye akili timamu
anadadisi mambo kwa kutaka kujua ukweli na uhalisia wa mambo hayo .
Alisema kuwa utashi wa kuelewa
mambo ni sehemu muhimu ya kujua mambo na kuweza kupanua ufahamu wa jambo
au taarifa kutoka katika sehemu husika .
Alifahamisha kuwa tamaduni na
malezi ya sehemu ndiyo yalikayoweza kumtayarisha mtoto au mwanajamii
kuwa na udadisi wa kutaka kujua hali halisi ya mambo yaliyomzunguka
kila siku katika dunia .
Akifahamisha kuwa social media
zimefahamu umuhimu huo wa kuweza kuwapatia habari kuhusu kujua wananchi
hali ambayo imeonyesha kupindukia kutokana na mitandao mingi kuelewa
dhamani ya kujua habari duniani .
Mwenyekiti huyo alieleza kuwa
maendeleo na mafanikio ya kupata taarifa kwa wakati imewezesha kutoa
kiu ya kujua na kuondoa utashi wa wananchi wa kutaka kujua kwa haraka
na kupata ufumbuzi.
“kujua jambo ni ufumbuzi wa jambo’’alisema mwenyekiti
No comments:
Post a Comment