Pages

Monday, September 24, 2012

MAONI YA MDAU: MBUYU TWITE HAKUWA ANAHITAJIKA YANGA - ALISAJILIWA KUWAKOMOA WATANI TU


 
Hivi kweli usajili wa wachezaji katika vilabu vyetu unafanywa kulingana na mahitaji ya makocha ama matakwa ya watu fulani.
MFANO - Hivi usajili wa Mbuyu kwenda Yanga, Chombo kwenda Simba ni mahitaji ya makocha?
Nasema hivi kwasababu kwa sasa Yanga wanahaha jinsi ya kumtmia Twite kikosini huku tayari wakiwa na Canavaro na Yondan kama central defenders chaguo la kwanza kutokana kuelewana kwao. Hali hii inapelekea Twite acheze kiungo cha ukabaji ambapo sio nafasi yake halisi huku akisababisha Chuji, Kijiko kukaa benc hi.
Twite amekuja kucheza Yanga na si kukaa benchi na hili kila shabiki wa Yanga analijua hi inamana kwamba tukiwa tunamuona uwanjan basi tujue kati ya Yondan au Cannavaro hatutawaona ama wakiwapo hao, basi ChujI na kijiko hawatakuwepo ili wampishe Twite no.6.
Hapo ndipo tunaona Yanga inazidiwa katika sehemu ya kiungo kwa kuwepo mtu ambaye hachezi vizuri nafasi hiyo.  Please viongozi wa soka Bongo achienI makocha na benchi la ufundi wachague wachezaji wanaowataka na wenye manufaa kwenye timu na sio kununua wachezaji kwa kukomoana na mashindano ya fedha msizonazo. Badilikeni jamani mnazidi kuliua soka la Bongo - by Fadhili Tabwene wa Kilosa MOROGORO.
source http://www.shaffihdauda.com/

No comments:

Post a Comment