MOTO mkubwa umezuka na
kuteketeza mabweni mawili ya wanafunzi zaidi ya 40 katika Shule ya Sekondari St
Marys iliyopo kata ya limuli,
Ifunda mkoani Iringa , inayomilikiwa na
Kanisa la katoliki jimbo la Iringa.
Katika tukio hilo hakuna
mwanafunzi aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hiyo licha ya moto
huo kuunguza magodoro, vitanda, nguo za wanafunzi pamoja na vifaa mbalimbali. Ajali
hiyo ilitokea mwishoni mwa wiki saa
mbili asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani na wengine nje ya bweni
Mwalimu mkuu wa shule
hiyo matulinus Kipupwe anaeleza kuwa ajali hiyo ni ya mara ya pili
ambapo nyingine iliwahi tokea mwezi wa saba mwaka huu na kuteketeza baadhi ya
mali.
Kipupwe ameongeza kuwa
ajali ya moto ilitokea mnamo tarehe 15 septemba muda wa saa mbili asubuhi na
kuharibu mali ambazo zinagharimu kiasi cha shilingi milioni 80 na kutaka
kuundwa kamati ambayo itashughulikia chanzo cha moto huo pamoja na wizi wa mali
za shule.
Katika hatua nyingine,
mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine ishengoma
alipotembelea shule hiyo alishangazwa na matukio ya moto huo kujitokeza
mara kwamara na kuwataka wananchi kuwafichua watu wanahusika na kuzuka kwa moto
huo.
“Tunabahati hatuna
mwanfunzi aliyepatwa na tatizo katika ajali hiyo lakini ni lazima tujiulize
nini tatizo la kuwepo kwa tatizo hili mara kwa mara”alisema
Dkt Ishengoma ameutaka
uongozi kufanya jitihada kwa muda wa siku kumi na kuhahakikisha wanafunzi
wanarudi ili kuendelea na masomo yao.
Wakitoa maoni yao mbele
mkuu wa mkoa Dkt Ishengoma wananchi
ambao walielekeza hisia zao kutokana na kile kinachosemekana ajali hizi
za moto katka shule hiyo zinahusishwa na masuala ya imani za kishirikina kwani
walipomaliza zima moto huo uliwaka tena pasipo kufahamu aliyewasha.
Mmoja wa wananchi
alieleza kuwa ana wasiwasi na ajali hizi za moto kwani msitu uko mbali sana na
shule hiyo na kueleza labda kuna mbinu zinazotumika ambayo zinahusishwa na
imani za kishirikina.
Naye diwani wa kata ya
lumuli charles luteto ameeleza kuwa amekaa na wananchi wake na kuomba kufanyika
uchunguzi kuhusu wakuu wa shule ambayo wamepita katika shule na kujaribu
kufahamu kuhusu mahusiano yao pamoja na malipo yao au kutoridhika na kuwa na
kinyongo toka kwa watu hao. Wananchi hao pia walisema yawezekana kuna mambo ya
kiini macho yanayofanyika ambayo kwa hali ya kawaida hayawezi kubainika.
Chanzo cha moto huo
hakijajulikana hivyo wameunda tume ili kufanya kazi hiyo na kutoa tathmini ya
hasara iliyojitokeza kuwa ni zaidi ya shilingi mill 80 .
Kutokana na hali hiyo
wanafunzi 376 wa shule hiyo wamelazimika kurudi nyumbani ili urekebishaji na
ujenzi unaogharimu zaidi ya shilingi milioni 80 ufanyike.
Huku zikiwa zimebaki
siku chache kwa wanafunzi walio kidato cha nne kuingia katika mitihani yao ya
taifa itakayoanza tarehe 8 oktoba mwaka huu.
Mabweni yakiwa yameteketea kwa moto pamoja na mali zilizokuwemo
No comments:
Post a Comment