Okwi |
Na Mahmoud Zubeiry
YUKO tayari
Dar es Salaam na keshokutwa atacheza- huyo si mwingine bali ni mshambuliaji hatari
wa Simba SC, Emanuel Arnold Okwi ametua leo Jijini kutoka Zambia, ambako
aliichezea timu yake ya taifa, Uganda, The Cranes mechi ya kuwania tiketi ya
kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Afrika Kusini jana na kufungwa 1-0
kwa mbinde.
Okwi ametua Uwanja
wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa 1:00 usiku huu na moja kwa
moja kuingia kambini, hoteli ya Sapphire, Kariakoo ambako klabu yake, Simba SC imejituliza
ikijiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC keshokutwa, Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Okwi hajaichezea
Simba mechi yoyote tangu msimu huu uanze, kutokana na pilika zake za kujaribu
kuhamia Ulaya, ambazo hazikufanikiwa.
Okwi alikaribia
kujiunga na FC Red Bull Salzburg ya Wals-Siezenheim, Austria baada ya kufuzu
majaribio ya wiki tatu, lakini klabu huyo ikaghairi dakika za mwishoni akarejea
nchini.
Kukwama kwa
Okwi kuliikosesha Simba Euro 600,000 ambazo klabu hiyo, ilikuwa tayari kutoa
kumnunua.
Awali, Simba
ilipata ofa ya kumuuza Okwi kwa Sh. Bilioni 2 kwa klabu ya Mamelodi Sundown ya
Afrika Kusini, lakini mshambuliaji huyo akasema anataka kwenda Ulaya.
Awali Olando
Pirates ya Afrika Kusini ilimuomba Okwi akafanye majaribio huko kama angefuzu
wangemsajili dau la dola 550,000 kabla ya kuibuka kwa taarifa za kutakiwa
Italia na klabu ya Parma.
Sasa Simba
inamsubiri mshambuliaji wake mmoja tu, Mzambia Felix Sunzu ambaye kwa wiki
nzima yuko kwao kwenye msiba wa dada yake, ambaye naye anatarajiwa kutua nchini
wakati wowote.
source http://bongostaz.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment