Pages

Wednesday, September 26, 2012

RAIS MUSEVENI ATANGAZA KUACHA KUSALIMIA KWA KUSHIKANA MIKONO NA WATU IKIWA NI TAHADHARI DHIDI YA EBOLA.



Rais Yoweri Museveni wa Uganda (pichani) ametoa wito kwa wananchi wa nchi hiyo kuwa waangalifu na afya zao akisema kuwa mengi kati ya magonjwa yanayosumbua nchini Uganda yana epukika na kudhibitika iwapo jamii itahasishwa zaidi.
Amesema kwa sasa ana umri wa miaka 68 na moja kati ya vitu ambavyo hana bajeti navyo ni maradhi.
Ameongeza kuwa hiyo ni kwa sababu yeye ni mtu makini na hapendi mazingira yatakayofanya ashindwe kufanya jambo lolote kwa sababu ya kuumwa.
Rais Museveni amesema tofauti na ugonjwa kama Mafua ambao unaambukiza kwa njia ya hewa, Ukimwi ni ugonjwa ambao watu wanautafuta na kuusambaza kwa wengine.
Ametaja tatizo linguine kuwa ni unywaji wa pombe, akishangazwa na tabia za baadhi ya watu kunywa pombe mpaka mashavu yanavimba, na kufafanua kuwa kama yeye angekuwa mnywaji pombe asiweza kuwatumia wananchi wake kwa kipindi chote hicho.
Katika hatua nyingine rais Museveni amesema kuwa siku hizi hasalimiani na watu kwa kushikana mikono bali hupunga tu.
Amefafanua kuwa hatua hiyo ni tahadhari dhidi ya uhonjwa hatari wa Ebola.

No comments:

Post a Comment