Soccer city Johannesburg South Africa.
Timu ya taifa Taifa stars
imepangiwa kucheza na Uganda (The Cranes) kwenye raundi ya kwanza ya
michuano ya kuwania ticket ya kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wa
ndani (CAN) zitakazofanyika Afrika Kusini 2014.
Ratiba iliyopangwa sept 7 2012
kwenye makao makuu ya shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) mjini
Cairo inaonyesha Tanzania imeingia moja kwa moja raundi ya kwanza ambapo
itacheza na Uganda.
Mechi ya kwanza itachezwa
uwanja wa taifa Dar es salaam kati ya june 21,22 na 23 2013 wakati
marudiano itakua uwanja wa Mandela Namboole jijini Kampala kati ya july
5,6 na 7 2013.
Nchi 38 zinashiriki kwenye hizo
mechi za mchujo ambapo nyingine zitaanzia raundi ya awali itakayochezwa
kati ya november 30 na december 1 na 2 mwaka huu wakati mechi za
marudiano zitakua kati ya December 14, 15 na 16.
Ratiba imepangwa kwa makundi ya
kanda ambapo jumla ya timu 16 ndizo zitakazocheza fainali hizo nchini
Afrika kusini, kanda ya kaskazini itapeleka timu mbili katika fainali,
kanda ya magharibi A pia timu mbili, Magharibi B timu tatu, Kanda ya
kati timu tatu, Kanda ya kati mashariki timu tatu, kanda ya kusini timu
tatu akiwemo mwenyeji Afrika Kusini.
Kwa upande wa kanda ya Tanzania
(Kati mashariki) timu zinazoanzia raundi ya awali ni Burundi, Eritrea,
Ethiopia na Kenya ambapo kama hufahamu fainali za kwanza za CAN
zilifanyika Ivory Coast 2009 ambapo Tanzania ilishiriki lakini mshindi
alikua Congo DRC na fainali za pili zilifanyika 2011 nchini Sudan ambapo
Tunisia ndio ilichukua ubingwa.
Fainali za kwanza zilishirikisha timu nane kabla ya kuongezwa hadi 16 za sasa.
No comments:
Post a Comment