Spika
wa Bunge Mhe. Makinda akiwasili katika hotel ya The Grand Cinnamon mara
baada ya kushuka katika basi maalum lililomchukua yeye na ujumbe wake
kutoka uwanja wa ndege mchini Colomo Sri Lanka
Afisa
Dawati la CPA katika Bunge la Tanzania Ndg. Said Yakubu akimpokea Mhe.
Spika mara baada ya kuwasili mjini Colombo Sri Lanka kuhudhuria Mkutano
wa 58 wa CPA. Katikati ni kamimu Katibu wa CPA kanda ya Afrika na Mkuu
wa Sehemu ya Itifaki na uhusiano wa Kimataifa kutoka Bunge la Tanzania
Ndg. Dimitries Mgalami
Ndg. Dimitries Mgalami akimsindikiza Mhe. Spika katika hotel itakayofikia wakati wote wa Mkutano huo wa CPA
kamimu
Katibu wa CPA kanda ya Afrika na Mkuu wa Sehemu ya Itifaki na uhusiano
wa Kimataifa kutoka Bunge la Tanzania Ndg. Dimitries Mgalami akiteta
jambo na Mhe. Spika mara baada ya kumpokea alipowasili Colombo Sri Lanka
kuhudhuria Mkutano wa mwaka wa CPA unaofanyika Nchini humo kuanzaia
tarehe 7 hadi 15 Septemba, 2012.
Mjumbe
wa CPA tawi la Tanzania Mhe. Zitto Kabwe akiteta jambo na Mhe. Okupa
Elijah kutoka Bunge la Uganda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa
ndege colombo Sri lanka kuhudhuria mkutano wa 58 wa CPA. aliyeko pembeni
ni Mbunge kutoka Uingereza.zote na Owen Mwandumbya wa Bunge
---
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda amewasili Mjini Colombo nchini Sri Lanka
kuhudhuria Mkutano wa 58 wa Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya
Madola Dunian (CPA). Mkutano huo wa mwaka unafanyika Nchini humo
kuanzaia tarehe 7 hadi 15 Septemba, 2012, ambapo zaidi ya wabunge 1000
na Maspika wa Mabunge zaidi ya 80 kutoka nchi mbalimbali wananchama wa
jumuiya ya Madola watahudhuria mkutano huo wa mwaka.
Ujumbe
wa Tanzania katika Mkutano huo unaongozwa na Mhe. Spika ambaye pia
ataongoza wabunge wengine kutoka tawi la CPA Tanzania ambo ni Mhe. Ziito
Kabwe, Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mhe. Beatriace Shelukindo, Mhe. Hamad
Rashid Mohamad na Mhe. Muhonga Ruhanya ambapo jumla ya mada 9
zinatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment