Pages

Sunday, September 30, 2012

TANESCO SINGIDA YAWATAKA WANAHABARI KUSHIRIKIANA NAYO KUKABILI WEZI WA UMEME.



Meneja wa TANESCO mkoa wa Singida Maclean Mbonile akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya mkakati wa uboreshaji wa huduma za shirika hilo. (Picha na Nathaniel Limu).
Meneja wa shirika la TANESCO mkoani Singida Maclean Mbonile amewaomba waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuhamsisha wananchi washiriki kutoa maoni yao yatakayosaidia uboreshaji wa huduma za TANESCO ili ziweze kukidhi mahitaji ya wateja.
Meneja Mbonile ametoa changamoto hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, juu ya mchakato wa kufanya mabadiliko ya kimuundo na kiutendaji kwa lengo la kuboresha huduma za TANESCO.
Akifafanua, amesema shirika la TANESCO linakusudia kufanya mabadiliko makubwa ya uboreshaji wa huduma zake, ili shirika liweze kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wateja wake kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Amesema ili  uboreshaji huo wa huduma uweze kufanikiwa kwa kiwango cha juu, wananchi na wateja hawana budi kushiriki kutoa maoni yao juu ya TANESCO mpya iweje.
Aidha, amesema kila mtoaji wa maoni hayo, anatakiwa kuandika namba yake ya simu, ili endapo ufafanuzi zaidi utahitajika, mhusika aweze kupatikana kwa urahisi.
Katika hatua nyingine, Mbonile amewataka waandishi wa habari kushirikiana na TANESCO katika mapambano dhidi ya wezi wa umeme.
Amesema asilimia 30 ya umeme wa TANESCO, unaibwa na wahalifu kwa njia ya kujiunganishia umeme na wengine kuchezea mita.

No comments:

Post a Comment