Na Raphael Okello, Bunda
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Bw. Stephen Wassira,
amesema Serikali ina uwezo wa kumuomba Msajili wa Vyama vya Siasa
nchini, Bw. John Tendwa ili akifute Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), kama kitaendeleza siasa za kuvuruga amani ya nchi.
Alisema
Watanzania walikubali mfumo wa vyama vingi kwa nia njema ya kuleta
demokrasia ya uhuru wa kutoa maoni na kulumbana kwa hoja bila kuvuruga
amani, utulivu au kufanya uchochezi.
“Katiba
ya nchi inatoa haki kwa vyama vyote vya siasa kufanya maandamano na
mikutano ya hadhara kwa kuzingatia taratibu na sheria ya nchi badala ya
kujiamulia na kufanya fujo,” alisema.
Aliongeza
kuwa, uhuru wowote una mipaka yake kwani sheria hairuhusu kila mtu,
kikundi cha watu au chama chochote kufanya wanavyoona inafaa na kutoa
shutuma za kichochezi.
“Watanzania
wanapaswa kuelewa kuwa, Seriokali ina uwezo wa kuipa CHADEMA kadi ya
njano na kama itaendelea kucheza rafu uwanjani, itapewa nyekundu.
“Sisi tulipewa dhamana na wananchi ili kulinda amani, utulivu na
mshikamano
wa Taifa, hatupo tayari kuvumilia vitendo visivyokoma vya kuvuruga
amani na utulivu....tunaiomba CHADEMA waheshimu sheria ya mchezo vyama
vingi,” alisema.
Bw.
Wassira ambaye anafanya ziara ya kutembelea wapiga kura jimboni kwake,
aliyasema hayo wakati akijibu maswali ya wakazi wa Kijiji cha Bukama,
Kata ya Nyamuswa, wilayani Bunda.
Wakazi
hao walitaka kujua Serikali kama walizni wa amani na utulivu wa nchi
inaonaje mwenendo wa CHADEMA ambapo swali hilo liliulizwa na Bw. Samwel
Msika, mkazi wa Kijiji cha Bukama.
“Wewe
Bw. Wassira ni miongoni mwa viongozi Serikalini, hivi sasa umesema
Serikali inahimiza amani, mshikamano na utulivu wa nchi, je mwenendo wa
CHADEMA kufanya fujo mnauonaje ni salama, mmeukubali, mnauunga mkono au
mnauzungumziaje,” alihoji.
Wakazi
wengine wa kijiji hicho, walimtaka Bw. Wassira kutoa ufafanuzi juu ya
kanuni za Bunge kama zinatoa fursa kwa wabunge kutoa maneno ya kashfa
kwa kiongozi wa nchi.
Walidai
ni hatua zipi ambazo zinachukuliwa kwa baadhi ya wabunge wanaotoa
maneno hayo kwani wapo baadhi yao ambao hivi karibuni walifanya hivyo
bungeni mjini Dodoma.
“Tunataka
kujua msimamo wa Serikali na hatua zinazochukuliwa kwa baadhi wa
viongozi serikalini pamoja na wabunge ambao hivi karibuni walidaiwa
kujihusisha na vitendo vya rushwa na kuficha fedha za umma nje ya nchi,”
alisema.
Akijibu
hoja hizo, Bw. Wassira alisema pamoja na mambo mengine, kanuni na
miongozo ya Bunge inakataza wabunge kutoa kauli za kashfa dhidi ya Rais
na mbunge anayefanya hivyo, anachukuliwa hatua na Kamati ya Maadili ya
Bunge.
Alisema
zipo taratibu za kujadili utendaji wa Rais bungeni kwa Spika kupelekewa
hoja badala ya kutoa maneno ya kashfa. Kuhusu mafisadi alisema
uchunguzi unaendelea na wote ambao ushahidi wao utapatikana
watashtakiwa.
Aliongeza
kuwa, Serikali imekuwa ikichukua hatua ambapo hadi sasa, wapo baadhi ya
Mawaziri ambao wamefikishwa mahakamani akiwataja Bw. Daniel Yona na Bw.
Bazir Mramba na kuhadharisha wananchi kutofanyia kazi uzushi na chuki
binafsi za wanasiasa.
SOURCE MAJIRA
No comments:
Post a Comment