UTENDAJI
kazi usiyofuata kanuni katika pantoni za Serikali Kigamboni, umeelezwa
kuwa ndiyo chanzo cha kuzorota huduma na kusababisha usumbufu kwa
wananchi wanaotaka kuvuka nyakati za asubuhi.
wakazi hao walisema pale Feri kumekuwa na miungu watu wanaofanyakazi wanavyotaka bila kujali haki za watu wengine.
Walisema
utakuta wafanyakazi hao wa pantoni hizo kwa makusudi huamua kufanyakazi
kwa kutumia pantoni moja baadala ya vyote viwili kitendo ambacho
husababisha msongamano wa biria na magari.
Mmoja
wa wakazi wa Kigamboni, Daina Christopher, alisema usumbufu wanaoupata
kutoka kwa wafanyakazi wa vivuko hivyo unawafanya hadi baadhi ya watu
wengine kufikiria kuhamia mjini.
“Mimi
nashangaa sana kwani utakuta wafanyakazi hao kwa utashi wao wenyewe
wanaamua kupunzisha pantoni moja eti wakidai kuwa wanabana gharama za
mafuta kitendo ambacho hakieleweki”alisema Daina.
Alisema
kama serikali imewaagiza hivyo kutumia kivuko kimoja basi itambuwe kuwa
haiwatendei haki kwa kuwa utaratibu huo umekuwa ukisababisha usumbufu
kwa wananchi kuchelewe katika majukumu yao ya uzalishaji kipato.
Naye
Khamisi Halid hapendezwi na utaratibu unaofanywa na wafanyakazi katika
pantoni hizo pale wanapotumia mashine mbili huku nyingine mbili
zikizimwa kwa makusudi ili mafuta yake wayachukuwe kwa maslahi yao
binafsi.
Alisema
wafanyakazi hao wamekuwa wakifanya hujuma mbalimbali lakini cha
kushangaza hata wanapopiga kelele kwenye vyombo vya habari hakuna hatua
za uwajibishaji zinazotekelezwa.Endelea kupitia audifacejackson
blogspot..“Mwandishi
naona unajisumbua kwani wewe siyo wa kwanza, wamekuaja wengi na
tumewaeleza kama haya lakini bado wanatutesa haiwezekani pantoni ziko
mbili lakini kwa makusudi wanaamua kutumia moja ili mradi waibe mafuta
sasa sisi tunawaachia nyinyi vyombo vya habari”alisema.
Fullshangweblog
ilipouliza kuhusu madai hayo kwa baadhi ya wafanyakazi wa pantoni hizo
kila moja aliruka wakidai kuwa wao si wasemaji.
“Pamoja
na kuwa sisi siyo wasemaji lakini madai hayo yanalengo la kutuharibia
kazi zetu”alisikika mmoja wawafanyakazi hao akisema bila kutoa
ufafanunuzi kuhusu ucheleweshaji wa kuwavusha wananchi huku akikataa
kutaja jina lake.
No comments:
Post a Comment