Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari,Vijana na
Utamaduni Tanzania Profesa Hermas Mwansoko akitoa maelekezo kwa wajumbe
wa Jumuiya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki
Kamishna wa Utamaduni Zanzibar Hamad Bakar Mshindo (kulia) akitoa
maelezo ya Jengo hilo ambalo ndio Makao makuu ya Jumuiya ya Kamisheni ya
Kiswahili ya Afrika Mashariki
Picha
ya pamoja ya wajumbe wa Jumuiya ya Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika
Mashariki katika Makao makuu iliyoteuliwa leo Eacrotanal Mjini
Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
Kuwepo kwa Makao makuu ya Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mjini Zanzibarkutasaidia kukuza Lugha ya Kiswahili,Utamaduni na Michezo kwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
Hayo
yameelezwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Tanzania Profesa
Hermas Mwansoko katika ukumbi wa Eacrotanal wakati walipokuwa wakijadili
uanzishwaji wa Makao makuu ya kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki na kuangalia Itifaki ya kuanzisha Kamisheni ya
Utamaduni na Michezo.
Amesema
kuwa Zanzibar ni chimbuko la Kiswahili sanifu hivyo ni vyema kuirejesha
historia ya kiswahili hapa nchini ili kiweze kukuwa zaidi na kuwepo
muendelezo mzuri wa lugha, utamaduni na michezo kwa nchi wanachama wa
jumuiya hiyo.
Aidha Profesa Mwansoko amesema kuanzishwa kwa jumuiya hiyo Zanzibar kutatoa
nafasi za ajira kwa wazanzibari wenyewe kwani wataweza kupata ajira na
kuweza kutoa wataalamu wazuri wa lugha ya Kiswahili jambo ambalo
litapelekea maendeleo nchini.
Amefahamisha
kuwa, kuwepo kwa makao makuu hayo hapa nchini kutaweza kudumisha
mashirikano ya karibu kwa wanachama wa Afrika Mashariki katika mambo ya
utamaduni na michezo.
Aidha
alisema lengo la mkuutano huo ni kuleta wataalamu wa lugha na utamaduni
ili kuweza kujadili kuhusu utamaduni na michezo katika nchi za Jumuiya
Afrika ya Mashariki ambazo zitaweza kukuza utamaduni wake na kujipatia
maendeleo na kuepukana na umasikini katika nchi hizo.
Akielezea
kuhusu mijadala Profesa Mwansoko amesema kuwa Jumuiya hiyo itajadili
marekebisho ya uanzishwaji wa kamisheni ya Utamaduni na michezo na
kuweza kufikia lengo iliyojiwekea jumuiya hiyo.
Kwa
upande wao washiriki wa Mkutano huo wameishukuru Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar kwa ushirikiano wao na kuweza kukubali Makao makuu ya
Kamisheni hiyo kuwepo Zanzibar na kutoa fursa nzuri ya kukikuza kiswahi
katika nchi za Afrika ya Mashariki.
Jumuiya
hiyo itakuwa na makao makuu yake hapo Eacrotanal mjini Zanzibar ambapo
wanachama wote kwa pamoja walikubaliana na kuridhika kuwepo kwa makao
makuu hayo katika eneo bila pingamizi yoyote.
Mkutano
huo wa wiki moja ambao utajadili mada mbalimbali zinazohusiana na
utamaduni, michezo na lugha ambao umewashirikisha wanachama kutoka
Burundi, Kenya, Uganda, Rwanda na Tanzania.
No comments:
Post a Comment