Mbunge
Amos Makalla, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, kusikiliza kero za wananchi , Kijiji cha Kibagara
Kukata utepe ikiwa ni ishara ya kuzinduzi wa Ofisi ndogo ya Mbunge wa Jimbo la Mvomero_
Wananchi wa Kata ya Langali, Wilaya ya Mvomero, wakisubiri kumsililiza mbunge wao Amos Makalla.
Wananchi
wa Kijiji cha Kibagara, Kata ya Tchenzema ,Wilaya ya Mvomero,
wakimkabidhi zawadi ya mbuzi 'nyama' Mbunge wao Amos Makalla ( mwenye
suti kulia
Wananchi
wa Kijiji cha Kibagara, Kata ya Tchenzema , Wilaya ya Mvomero
wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo hiyo, Amos Makalla ( hayupo pichani)
Septemba 22, mwaka huu.
Mbunge
wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Septemba 22, mwaka huu, alifanya
ziara katika Kata ya Langali pamoja na Tchenzema, zilizopo Tarafa ya
Mgeta, Wilayani Mvomero.
Akiwa
katika Kijiji cha Kibagara, Kata ya Tchenzema, Mbunge huyo pamoja na
kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kujitolea majawabu na
ufafanuzi , pia aliahidi kutoa mifuko 50 ya safuji kwa ajili ya ujenzi
wa Zahanati ya Kijiji hicho ili itakapokalimika iwezekuwaondolea tatizo
la kusafiri umbali mrefu kwenda kupata tiba.
Katika
Kata ya Langali, Mbunge huyo alishiriki hafla ya uzinduzi wa Ofisi
ndogo ya Mbunge wa Jimbo hilo baada ya kukotisha Nyumba na kuifanyia
utarabati mkubwa na kulipoia karo ya kipindi cha miaka mitano , ili
iwezekutumika kuwahudumia wananchi wa Tarafa ya Mgeta , kufikisha kero
zao kwa Katibu wa Mbunge wa Tarafa na baadaye kuzifikisha kwa Mbunge.
Pia
Ofisi hiyo itakuwa ni sehemu ya uratibu wa ziara ya Mbunge wa Jimbo
wakati wa kutembelea Vijiji vya Kata zilizopo kwenye Tarafa ya Mgeta.
Akizundua
Ofisi ndogo hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka ,alimpongeza
Mbunge huyo juu uamuzi wake wa kufungua Ofisi katika Tarafa hiyo
akionesha mfano wa kuingwa na Wabunge wengine , kuwasongezea huduma ya
karibu wananchi , ambapo Ofisi hiyo mbali na kutumiwa na Mbunge ,
Serikali ya Wilaya itakuwa bega kwa bega kuwez kupata maoni ya wananchi
na kero zao zitakazofanyiwa kazi kwa haraka kupitia Ofisi hiyo
No comments:
Post a Comment