Balozi Maalumu wa Umoja wa Posta Duniani, Mh. Prof. Anna Tibaijuka akiwasilisha Tamko la Umoja wa Posta Duniani la Kutoa Anwani za Makazi KWA watu wote duniani.
Ujumbe wa
Tanzania kwenye Mkutano Mkuu wa 25 wa Umoja wa Posta Duniani
ukimsikiliza Mh.Prof. Anna Tibaijuka akiwasilisha Tamko la UPU kuhusu
anwani za Makazi. Ujumbe huo unaongozwa na Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, Mh. Prof. Makame Mbarawa,wa pili kulia. Wengine
ni Prof. John Nkoma, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, wa kwanza kushoto, Prof.
Patrick Makungu, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, (wa tatu toka kutoka kulia, anayefuata ni Bwana Deos Mndeme,
Postamasta Mkuu Tanzania, anayefuata ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi TPC Dr. Yamungu Kayandabila, anayefuata Kaimu Mwenyekiti wa
Bodi ya TCRA na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Uchukuzi
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dr. Vuai Lila na mwisho ni Mkurugenzi wa
Huduma za Posta TCRA.
Wawakilishi
wa nchi mbalimbali duniani wakimsikikiliza Balozi Maalum wa Umoja wa
Nchi wanachama wa UMoja wa Posta Duniani akiwasilisha Tamko la Umoja wa
Posta Duniani la Kutoa Anwani A Makazi KWA watu wote duniani.
Na Innocent Mungy - Doha, Qatar
Balozi
Maalumu wa Umoja wa Posta Duniani, Mh. Prof. Anna Tibaijuka, ameyahimiza
Mataifa yote duniani kuhakikisha wanaboresha maisha ya watu wake kwa
kuweka anwani za makazi na posti kodi zenye kukidhi mahitaji mbalimbali
ya maendeleo ya raia wake.
Akiwasilisha
Tamko la Doha La Umoja wa Posta Duniani la Kutoa anwani kwa watu wote,
Mh. Tibaijuka ambae pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, amezishauri nchi wanachama wa UPU kuhakikisha kila raia
anatambuliwa alipo na kuhakikishiwa usalama wake na kujumuishwa kwenye
mipango ya maendeleo ya nchi yake.
Amesema,
watu kukosa anwani za makazi kunawakwamisha katika shughuli za maendelo
kama vile uwezo wa kutambuliwa ili kupata huduma za msingi za maisha yao
kama vile shule, maji na huduma mbalimbali za jamii. Amezitaja huduma
zingine kuwa ni pamoja na utambulisho wa makazi rasmi ili kuweza kupata
mikopo kutoka katika mabenki yanayoshindwa kutoa mikopo kutokana na
wengi wa raia kukosa utambulisho wa wanakokaa.
Aidha
amesema, kutokana na watu wengi zaidi kuhamia mijini kutoka vijijini,
Serikali hazina budi kujipanga kupitia program za mipango miji ili
kudhibiti makazi holela ambayo hayawezi kutambuliwa rasmi kutokana na
kutokuwa na miundo mbinu yeye ubora KWA maisha ya watu.
Prof.
Tibaijuka pia amezihimiza nchi wanachama wa UPU kuwekeza katika kuwa na
mfumo thabiti wa anwani za makazi na posti kodi ili mfumo huo uwezo
kuboresha maisha ya watu hata kwa huduma za afya za dharura, usalama na
urahisi wa kutoa huduma za uokoaji wa watu wakati wa dharura.
Mh.
Prof. Tibaijuka amesema Tanzania tayari imeanza kutekeleza programu wa
anwani za makazi na imedhamiria programu hii kukamilika kwa mafanikio
makubwa. Tayari miji ya Arusha na Dodoma imeanza utekelezaji wa
majaribio na hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
alizindua utekelezaji wa utoaji wa anwani za makazi KWA mkoa wa Dar es
salaam ambapomaliwaagiza watendaji wa jiji la Dar es salaam kuanzia
kutoa majina KWA MTAA yore jijini.
Nchi
mbalimbali zimezungumza kufungua mkono Tamko hilo, ikiwemo Costarica
iliyopendekeza kuwashurikisha wananchi, wafanyibiashara na taasisi
mbalimbali ili kufanikisha mpango wa anwani za makazi kwa kila mwananchi
duniani.
Leo
jioni, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. Prof. Makame
Mbarawa anatarajia kuhutubia mkutano huu kutoa taarifa ya maendeleo ya
huduma za Posta Tanzania na jinsi ya kukabiliana na changamoto
mbalimbali zinazoikumba sekta ndogo ya Posta duniani, hasa nchi kama
Tanzania.
No comments:
Post a Comment