Pages

Monday, October 8, 2012

AZAM YALETA KOCHA MWINGINE KUTOKA SERBIA


Bunjak


AZAM FC, washindi wa Medali tatu za Fedha, Ligi Kuu msimu uliopita, Kombe la Urafiki na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, wameimarisha benchi lao la ufundi kwa kuleta kocha mpya kutoka Serbia, Slobodan.
Slobodan ametua Azam kwa kazi moja tu maalum, kuwanoa makipa wa timu hiyo inayofukuzana na Simba kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Slobodan ni chaguo la kocha wa sasa wa Azam, kutoka Serbia pia, Boris Bunjak ambaye amerithi mikoba ya Muingereza Stewart Hall aliyefukuzwa Julai mwaka huu.
Bunjak mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), alitua Azam, akitokea FC Damac ya Saudia Arabia aliyoanza kuifundisha mwaka jana na kabla ya hapo alifunisha klabu za kibao, zikiwemo FK Sloga Kraljevo, FK Javor Ivanjica, Crvena Zvezda Gnjilane, FK Radnicki Nis, FC Uralan Elista, FK Mladi Radnik, FK Crvena Zvezda Beograd, Al-Shaab, FK Hajduk Kula na Al-Nasr.
Awali, Bunjak aliyezaliwa Novemba 17, mwaka 1954 ( miaka 57), alicheza soka katika klabu za FK Sloga (Kraljevo), FK Vozdovac (Beograd), FK Radnicki (Kragujevac), FK Olimpia (Ljubljana), FK Sumadija (Arandjelovac), FK Sloga (Kraljevo), FK Borac (Cacak) na FK Sloga (Kraljevo).
Mserbia huyo anakuwa kocha wa tano Azam, ndani ya miaka minne tangu ianze kucheza Ligi Kuu, 2008 baada ya Stewart, Mbrazil Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin, Mbrazil mwingine.
Lakini ni Stewart angalau anaacha kumbukumbu ya taji na Medali za Fedha Azam, baada ya kuiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu, kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Mei mwaka huu, kabla ya kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame Julai mkwaka huu.
Bunjak alitambulishwa Azam Agosti 7, mwaka huu na akaanza kufundisha timu siku iliyofuata na hadi sasa amekwishaiongoza timu katika mechi 11 na kushinda saba, sare moja na kufungwa mbili, zote dhidi ya Simba SC moja kwenye Nusu Fainali ya Kombe la BancABC Sup8R 2-1 na nyingine ya Ngao ya Jamii 3-2.
REKODI YA BORIS BUNJAK AZAM
Azam 2-1 Polisi Moro              (BancABC)
Azam 1-2 Simba B                  (BancABC)
Azam 8-0 Transit Camp          (Kirafiki)
Azam 1-0 Prisons                   (Kirafiki)
Azam 2-0 Coastal Union        (Kirafiki)
Azam 2-3 Simba SC               (Ngao ya Jamii)
Azam 1-0 Kagera Sugar        (Ligi Kuu)
Azam 2-2 Toto African           (Ligi Kuu)
Azam 3-0 JKT Ruvu               (Ligi Kuu)
Azam 1-0 Mtibwa Sugar        (Ligi Kuu)
Azam 1-0 African Lyon         (Ligi Kuu) 
source http://bongostaz.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment