Pages

Sunday, October 28, 2012

BURKINA FC MDEBWEDO LIGI DARAJA LA KWANZA, YATANDIKWA NA MKAMBA RANGERS 1-0 JAMHURI MOROGORO.




 Mshambuliaji wa timu ya soka ya Mkamba Rangers Msafiri Makambi kulia akichuana na mchezaji wa Burkina FC, Saidi Manga wakati wa mchezo wa ligi daraja la kwanza uliowakutanisha timu zote za mkoa wa Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa ambapo katika mchezo huo Burkina ilifungwa bao 1-0.
Mshambuliaji wa timu ya soka ya Mkamba Rangers Msafiri Makambi kulia akichuana na mchezaji wa Burkina FC, Saidi Manga wakati wa mchezo wa ligi daraja la kwanza uliowakutanisha timu zote za mkoa wa Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani hapa ambapo katika mchezo huo Burkina ilifungwa bao 1-0.

TIMU ya soka ya Burkina FC imeendeleza kugawa pointi mbele ya Mkamba Rangers katika mchezo zote za Morogoro katika mkali wa ligi daraja la kwanza baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kikiwa ni cha pili mfululizo kwenye uwanja wake wa nyumbani mchezo uliofanyika uwanja wa Jamhuri mkoani hapa.

Mshambuliaji Athman Msafiri ndiye aliyezamisha jahazi la Burkina FC baada ya kuifungia timu yake bao katika dakika ya 76 kwa kichwa kufuatia mpira wa adhabu ndogo uliochingwa na Kamugisha Edson nje ya 18 kufuatia mlizni wa Burkina FC, Peter Damian kumfanyia madhambi mchezaji wa Mkamba Rangers na kufunga bao hilo lililomuacha Mohamed Barakati asijue la kufanya na mpira kujaa wavuvi.

Licha ya kupata kipigo hicho cha kupoteza mchezo wa pili pia kocha mkuu wa timu hiyo ya Burkina FC, Damian Mussa amejikuta akimaliza mchezo katika jukwaa la mashabiki baada ya kuondolewa katika benchi la ufundi na mwamuzi wa mchezo huo Mary Kapinga kutoka Songea dakika ya 44 kufuatia kutupiana maneno makali na mashabiki wake.

Katika mchezo huo Burkina FC walicheza chini ya uwezo wao na kusababisha kukaribisha mashambulizi ya mara kwa mara lango kwao baada ya kushindwa kucheza kwa maelewano huku Mkamba wakitumia nafasi hiyo kutengeneza mashambulizi kwa wapinzani wao.

Kocha mkuu wa Mkambara Rangers Keneth Mkapa alisema kuwa ushindi huo umempa faraja na kuongezea morali kwa wachezaji baada ya kupoteza mchezo wao wa ufunguzi na kufungwa bao 2-0 na Polisi Iringa wakati mchezo ujao ukitarajia kucheza na Small Kids ya Rukwa Oktoba 31 mkoani Rukwa huku Kocha wa Burkina akishindwa kupatiakana kuzungumzia mchezo huo.

Wakati Mkamba ikitarajia kucheza na Small Kids katika mchezo wa tatu yenyewe Burkina FC itachuana na Majimaji ya Songea Oktoba 31 kwenye uwanja wa Majimaji  mwaka huu baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza na Mbeya City kwa kupachikwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Jamhuri.

No comments:

Post a Comment