Meneja
wa kanda ya Kaskazini wa mfuko wa pensheni kwa wafanyakazi wa
Serikaliza mitaa LAPF Bw. Lulyalya Sayi akikabidhi mafuta ya kulainisha
ngozi kwa Ernest Kimaya Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania katika
hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi za kanda Makumbusho
jijini Dar es salaam, kulia ni Afisa Masoko wa LAPF Rehema Mkamba na
kushoto ni Mweka hazina wa Chama Cha Albino Tanzania Abdillah Omar.
Baadhi wa wanachama wa chama cha Albino Tanzania waliohudhuria katika hafla ya kukabidhi mafuta hayo
Mfuko wa
Pensheni wa LAPF leo umetoa msaada wa Lotion za Kuzuia Mionzi ya Jua kwa
wanachama wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi Dar es Salaam wenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni tano.
LAPF
inatambua madhara ya mionzi ya jua na pia umuhimu wa lotion hizi.
inatambua pia mahitaji ni makubwa zaidi lakini kwa kuanzia imetoa msaada
huu wa lotion 140 zenye ujazo wa 100 mls wenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni tano ikiamini kwamba zitasaidia kupunguza mahitaji
hayo. Kadhalika LAPF inawaomba msisite kuendelea kuwasilisha maombi hayo
na itasaidia kadri uwezo utakavyo ruhusu.
LAPF
imekuwa mstari mbele katika kusaidia makundi mbali mbali yenye ya watu
wenye mahitaji maalum katika jamii hasa watu wenye ulemavu wa ngozi.
Kama mtakumbuka mwaka juzi ilitoa msaada wa shilingi milioni tano kwa
ajili ya ujenzi wa boma kwa Mlemavu wa ngozi aliyekatwa mikono, mwaka
jana tulitoa msaada wa fulana na vifaa mbali mbali kwa chama cha wenye
ulemavu wa ngozi Dodoma na mwaka huu tukaona tuoe msaada huu wa lotion
za kulainisha ngozi
Mtambue
kuwa LAPF ni Mfuko wa Pensheni na wanachama wake ni mtu yeyote anaeamua
kujiunga na LAPF iwe ameajiriwa au amejiajiri mwenyewe. Hifadhi ya jamii
ni haki ya kila mtu hivyo tunawashauri ndugu zetu wenye ulemavu wa
ngozi mjiunge na Mfuko huu unaotoa mafao bora zaidi nchini. Kadhalika
LAPF imeanzisha mpango wa akiba wa hiari ambao unamfaa kila mtu na riba
yake ni ya ushindani hivyo mjiwekee akiba kwa faida ya baadae.
Mbali na
Mpango huo, LAPF inatoa Mafao ya Kustaafu, Mafao ya Warithi, Mafao ya
Ulemavu, Mafao ya Uzazi na Msaada wa Mazishi kwa mwanachama aliyefariki.
LAPF pia inatoa mikopo ya Nyumba kwa wanachama wanaokaribia kustaafu
pamoja na mikopo ya wanachama kupitia SACCOS zao. Hivi sasa Mfuko uko
kwenye hatua za mwisho kuanzisha Mafao ya Elimu.
No comments:
Post a Comment