Mtuhumiwa Pacficus akipelekwqa mahakamani chini ya ulinzi mkali
Mtuhumiwa
wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha
Channel Ten Daud Mwangosi leo amefikishwa tena katika Mahakama ya
Hakimu Mfawidhi ya Wilaya kujibu shitaka lilalomkabili.Huku akiwa chini
ya ulinzi mkali wa askari.
Akisomewa
shitaka lake na mwendesha mashtaka wa serikali Mkuu lilian Ngilangwa ,
amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni askari mwenye namba G2573 Pasificus
Cleophace Simoni (23) mkazi wa FFU Iringa, anakabiliwa na shitakala la
mauaji ya makusudi.
Amesema
mtuhumiwa huyo mnamo 02 Septemba mwaka huu katika kijiji cha Nyololo
Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi
kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa
ya jinai.
Mbele ya
Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness
Lyimo mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo
haiwezi kusikiliza kesi za mauaji.
Kwa
mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16
iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya
kukusudia kupewa dhamana.
Mtuhumiwa
amerudishwa mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na
kesi hiyo imeahirishwa hadi 7 Novemba mwaka huu itakapotajwa tena
mahakamani hapo.
Mtuhumiwa huyo aliletwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kaitka gari la polisi lenye number za usajili PT 1467.
Huku
waandishi wa habari wakizuiwa kupiga picha jambo lililosababishwa
kusukumwa kwa mwandishi wa majira Elias Ally na mmoja wa Polisi hao.
No comments:
Post a Comment