Mkurugenzi
wa Maisha Plus,Masoud Kipanya (kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa
Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB ,Imani Kajula (pili kulia)
,Mwakilishi wa Idara ya Kilimo wa NMB, Carol Nyangaro (wa pili kushoto)
na Meneja wa Mikopo Midogo ya Biashara, Mashaga Changarawe.
Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB,Imani Kajula (kulia)
akiwagawia jarida la NMB Financial Fitness baadhi ya wakinamama wa Mama
Shujaa wa Chakula katika kambi ya Maisha Plus, jarida hilo lina maelezo
mengi yanayohusu uelewa wa matumizi ya fedha.
Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB ,Imani Kajula (kushoto)
akiwasomea jarida la NMB Financial Fitness wakinamama wa Mama Shujaa wa
Chakula katika Kambi ya Maisha Plus, jarida hilo lina maelezo mengi
yanayohusu matumizi mazuri ya fedha.
Meneja
wa Mikopo Midogo ya Biashara, Mashaga Changarawe.akipata kinywaji
kwenye kibuyu alipowatembelea wakinamama shujaa wa chakula katika kijiji
cha Maisha Plus.
NMB ikiwa
wadhamini wakuu wa mpango wa mama shujaaa wa chakula, imewatembelea
washiriki wa mama shujaa wa chakula katika kijiji i cha Maisha Plus
na kuwapa elimu ya kifedha kupitia mpango wa NMB Financial Fitness.
NMB
kupitia mpango wa NMB Financial Fitness unaolenga kuongeza uelewa wa
matumizi mazuri ya fedha imepata fursa ya kuwaelimisha washiriki kuhusu
huduma za kifedha, uwekaji akiba, kupanga matumizi, matumizi mazuri ya
kifedha na mengine mengi.
Vilevile, Washiriki hao walielimishwa kuhusu Mikopo Midogo na kati ya kibiashara pamoja na mikopo ya kilimo. NMB
inaamini udhamini huo ni sahihi kutokana na kuwa utakuza kilimo na
kuwasaidia wakulima wadogo katika maisha, mapambano dhidi ya
njaa,umasikini na uhaba wa ajira miongoni mwa wanawake.
No comments:
Post a Comment