Rais Alpha Conde (pichani) wa Guinea amewafukuza kazi mawaziri 11 wa serikali yake katika mabadiliko ya kushtukiza  yaliyotangazwa Ijumaa jioni na televisheni ya taifa.
Taarifa kutoka ofisi ya rais haikubainisha sababu ya mabadiliko hayo, lakini hatua hiyo imekuja wakati wasiwasi unaongezeka juu ya uchaguzi wa wabunge uliyocheleweshwa.
Miongoni mwa mabadiliko muhimu ni uteuzi wa Waziri Mkuu wa zamani na mwanadiplomasia wa siku nyingi Francois Louceny Fall kuwa Waziri  wa Mambo ya Nje.
Katika mabadiliko hayo Waziri wa Kilimo Jean Marc Telliano na Waziri wa Ujenzi na Maendeleo ya miji Mathurin Bangura, ambaye anatuhumiwa kwa kujilimbikizia mali akiwa mtumishi wa umma wamefukuzwa kazi.