JUMLA ya
warembo 29 kati ya 30 wanaowania taji la REDDS MISS TANZANIA 2012 leo
wameanza ziara rasmi ya kutembelea Vivutio vya Utalii vilivyopo Kanda ya
Kaskazini katika mikoa ya Moshi, Arusha na Manyara.
Warembo
hao wakiongozwa na Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania, wakiwa katika
mikoa hiyo watatembelea vivutio hivyo na kuhamasisha jamii ya watanzania
kuwa na desturi ya kutembelea vivutio hivyo vyua ndani na kuhamasisha
utalii.
Pia
warembo hao watapata fursa ya kujifunza vitu mbalimbali kuhusiana na
masuala ya utalii. Oktoba 7, warembo hao watatembrelea Hifadhi ya Mlima
Kilimanjaro, katika lango kuu la kupandia Mlima huo la Marangu.
Aidha kwa
mujibu wa ratiba hiyo, inaonesha kuwa warembo hao watafanya tamasha la
Michezo mjini Arusha kabla ya kuelekea Monduli ambako Oktoba 8 watazuru
Kaburi la Waziri Mkuu wa Zamani, Hayati Edward Moringe Sokoine.
Mrembo
Fatma Ramadhani kutoka Kanda ya Elimu ya Juu akiangalia vijana wafanya
biashara wadogo wa bidhaa za mkononi kituo cha Chalinze.
Misosi ni muhimu bwana kwa warembo, hapa wakiwa Korogwe High Way wakipata kitu ile roho inapenda.
Hawa waliamua kushow love kabla ya kupata mlo wao.
Washiriki hawa wa Redds Miss Tanzania 2012 wao walisema waweke Nakadhalika katika Menu yaoo hapo sasa wana fanya mambo.
Mary Chizi aliamua kushow love na wahudumu wa jiko la msosi hapo High Way, yes mrembo lazima ujichanganye na uwe mtu wa watu.
Kila mmoja wao alikamatia chakula hakuna asiyekula labda ambaye amefunga.
Safari iliendelea kwa gari lililobeba warembo kushika barabara
Stori zikaendelea huku safari ya kuitafuta Moshi mkoani Kilimanjaro ikinoga.
Kunywa na kutafuna havikukoma na warembo wa Redds Miss Tanzania walijinafasi.
Tabasamu kwa mpigapi na Camera jamani
Wahenga
walinena "shibe mwana Malevya Njaa Mwana Malegeza" haya sasa Shibe
ikaleta Usingizi na hawa waliamua kulala kidogo kupunguza uchovu
wsafari.
No comments:
Post a Comment