Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti katika bustani ya Jumba la Rideau
Hall jijini Ottawa katika siku ya pili ya ziara yake rasmi nchini Canada
huku akishuhudiwa na Gavana Jenerali wa nchi hiyo Mhe David Johnson na
mkewe Mama Sharon Johnson Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la askari
shujaa katika bustani ya Confederation Square jijini Ottawa Alhamisi
Octoba 4, 2012
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara
baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la askari shujaa katika
bustani ya Confederation Square jijini Otttawa Alhamisi Octoba 4, 2012
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisimama wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania
ukipigwa mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la askari
shujaa katika bustani ya Confederation Square jijini Ottawa Alhamisi
Octoba 4, 2012. Mbele yake ni baadhi ya veterani wa kijeshi
waliohudhuria hafla hiyo.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara
baada ya kupokelewa katika Bunge la Seneti la Canada. Kulia ni Spika wa
Bunge hilo Mhe Noel Kinsella, anayefuatiwa na Waziri Mkuu wa Canada Mhe
Stephen Harper na Spika wa Bunge la wawakilishi la Canada (House of
Commons), Mhe Andrew Scheer pamoja na viongozi wengine wa bunge hilo
Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper
katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, ambapo viongozi hayo
wawili walifanya mazungumzo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi ya sanduku la Zanzibar (Zanzibar
chest) Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la
Seneti la nchi hiyo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa katika ofisi ya Spika wa Bunge la
Wawakilishi la Canada (House of Commons) Mhe Andrew Sheer. Spika huyu,
mwenye umri wa miaka 32, ndiye kiongozi kijana kuliko wote katika
historia ya nchi hiyo waliopata kuchaguliwa kuongoza bunge hilo.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Canada Mhe
Stephen Harper wakitembea kuelekea kwenye chumba cha mkutano kuongea na
wanahabari. Zuria jekundu na bendera za Canada za kiongozi wa nchi
husika huwekwa sehemu hiyo kwa heshima na wakati wa ziara ya kiongozi wa
nchi ya nje aliye katika ziara rasmi nchini humo
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Canada Mhe
Stephen Harper wakishudia uwekaji sahihi mkataba wa ushirikiano kati ya
Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mhe.
Bernard Membe na Waziri wa Canada katika Bunge la seneti la nchi hiyo

No comments:
Post a Comment