Mabingwa watetezi wa ligi kuu tanzania bara wameondoka mchana huu kuelekea Tanga kwa basi lao la kisasa tayari kuwakabiri Coastal union kwenye mchezo wa ligi kuu unaotarajiwa kupigwa jumamosi
katika safari hiyo timu ya Simba itawakosa nyota watano, Emanuel Okwi
ambaye amekwenda kujiunga na timu yake ya taifa, Uganda, Ramadhan Chombo
‘Redondo’ anayesumbuliwa na Malaria, Haruna Shamte, Hamadi Waziri na
Komabil Keita ambao ni majeruhi. Mrisho Ngassa aliyekuwa anaumwa Malaria amepona na yumo kwenye msafara
WAKATI
HUOHUO, uongozi wa Coastal Union ya jijini Tanga, umesema kiungo
mshambuliaji wake, Gabriel Barbosa, raia wa Brazil, anatarajia kuwasili
nchini kesho.
Barbosa
amesajiliwa na Coastal Union akitokea katika Klabu ya Letleatipo Santo
Cruise inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Brazil.Akizungumza, Katibu Mkuu wa Coastal, El Siagi Kassim, alisema Barbosa amechelewa kutua nchini kutokana na tatizo la usafiri linaloikumba nchi yao kwa watu wanaotaka kuja katika Bara la Afrika.
“Tunatarajia kumpokea Barbosa siku ya Alhamisi (kesho) kwa kuwa tayari tumeshafanya naye mawasiliano, lakini kilichokuwa kikimsumbua hadi kusababisha achelewe kufika ni tatizo la usafiri lililokuwepo nchini mwao, hasa kwa wale waliotaka kuja Bara la Afrika.“Mara baada ya kutua atajiunga na wenzake ili kuongeza nguvu katika safu yetu ya kiungo na ushambuliaji. Lengo ni kufanya vizuri na hatimaye kumaliza ligi katika moja ya nafasi tatu za juu,” alisema Kassim.
No comments:
Post a Comment