Amir Mhando, Katibu Mkuu wa Taswa
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimesikitishwa na taarifa za baadhi ya waandishi wa habari za michezo kupewa vitisho wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kazi.
TASWA imepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya waandishi wa habari za michezo wakidai baadhi ya wanachama wa Yanga a.k.a ‘Makomandoo’
wamewapa vitisho kabla na baada ya mchezo kati ya Kagera Sugar na Yanga
uliofanyika Jumatatu wiki hii Uwanja wa Kaitaba Bukoba.
Sekreterieti
ya TASWA ilifanya mawasiliano ya haraka na Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji, Onesmo Kapinga ambaye alikuwa mkoani Kagera na amethibitisha
pasi na chembe ya shaka kwamba vitisho hivyo vimewanyima fursa ya
kutekeleza majukumy yao ya kazi.
Tukio
hili limetuhuzunisha sana kwa sababu licha ya kuwajengea hofu baadhi ya
waandishi wa habari kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi
kikamilifu, lakini linaweza kujenga chuki zisizo na msingi kati ya klabu
hiyo na TASWA.
Wanachama
na mashabiki wa klabu kubwa hapa nchini Simba na Yanga wakubali
changamoto za viwanjani na wasitake kutafuta mahali pa kupeleka lawama
zao pale wanapoona matokeo mabaya kwa klabu zao.
Si
nia ya TASWA kutetea udhaifu kama upo kwa baadhi ya waandishi wa
habari, lakini tunaona kwa malalamiko yanayotolewa na baadhi ya
makomandoo hao kwa wanahabari si mazuri na hoja zao hazina mashiko ni
kutapatapa.
Tunauomba
uongozi wa Yanga uwakemee mashabiki wake waachane na mambo yasiyo na
msingi ambayo hayana manufaa kwa klabu hiyo na ulimwengu wa soka hapa
nchini. TASWA inataka wanahabari wawe huru kutekeleza majukumu yao na
hilo tuna hakika litafanyika.
Kamati
ya Utendaji ya TASWA inatarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki ijayo
kujadili suala hili la vitisho kwa wanahabari na pia itajadili masuala
mbalimbali ikiwemo kutaja mkoa utakakofanyika Mkutano Mkuu wa mwaka wa
chama.
Nawasilisha.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
11/10/2012
No comments:
Post a Comment